Nafasi Ya Matangazo

April 04, 2024

 

Naibu Waziri Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Hamis Mwinjuma akizungumza na wanahabari leo April 4,2024 jijini Dodoma wakati wa Uzinduzi wa Jezi za Timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu (Picha na Manase Madelemu)

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania Michael Kadebe akizungumza na wanahabari leo April 4,2024 kwenye Uzinduzi wa Jezi za Timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu (Picha na Manase Madelemu)

Jezi za timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu zilizozinduliwa leo April 4,2024 jijini Dodoma na Naibu Waziri Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Hamis Mwinjuma (Picha na Manase Madelemu)

Naibu Waziri Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Hamis Mwinjuma amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Michezo yote ya kipaumbele inapata nafasi sawa

Mhe.Mwinjuma amesema hayo leo April 4,2024 Jijini Dodoma wakati wa Uzinduzi wa Jezi ya timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu ya Tanzania.

"Tuna michezo takribani sita ya kipaumbele inabidi kuhakikishe inapata nafasi sawa kwa maana ya kupewa nafasi ya sehemu kama miundombinu ya michezo na kuwezeshwa kwa timu zetu"amesema

Aidha amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Kikapu ili kuhakikisha wanatengeneza mabadiliko chanya ya kuutoa mpira wa Kikapu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Kuhusu suala la Mpira wa Kikapu kuwa mchezo wa kimashindano kama ulivyo Mpira wa Miguu hapa nchini Mhe.Mwinjuma amesema kuwa ni jambo ambalo inabidi libaki kwenye akili za viongozi wote wanaohusika na jambo hili.

"Ukikaa hivi juu juu ukiwa hufatlia unaweza kufikiri mchezo wa Mpira wa Kikapu umekufa kabisa,lakini ukienda kwenye matukio ya Mpira wa Kikapu unaipata picha kwamba huu mchezo una wapenzi wengi na kuna jukumu la kuhakikisha unachezwa kwenye viwango ambavyo awali walivitarajia"amesema


Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania Michael Kadebe awali akimkaribisha mgeni rasmi ameishukuru Serikali kupitia Wizara yake ya Michezo na Baraza la Michezo Tanzania BMT kwa kuwapatia Ushirikiano wa kutosha na kuwapatia miongozo inayowawezeshakusimamia,kukuza na kuendeleza mchezo wa Mpira wa Kikapu nchini.

Aidha ametoa shukrani kwa kampuni ya Michezo ya Kajumulon ambayo imetoa ufadhili wa kutengeneza Jezi.

"Hatua hii inaashiria maono ya Watanzania mbalimbali waliopo nje wenye moyo wa Uzalendo katika kuinua viwango vya michezo ikiwemo Mpira wa Kikapu katika nchi yetu"amesema

Kuhusu Jezi hizo Kadebe amesema kuwa ni zaidi ya kitambaa na muundu inajumuisha ndoto,matarajio,na bidii ya wachezaji wanaojitolea kwa mchezo wanaoupenda

Katika hatua nyingine Kadebe amewaambia wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu wavae jezi hiyo kwa kujivunia.

"Cheza kwa mapenzi na usisahau kamwe fursa na wajibu unaokuja na kuiwakilisha Tanzania yetu pendwa chini ya Rais wetu mpendwa"amesema

Posted by MROKI On Thursday, April 04, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo