Nafasi Ya Matangazo

April 16, 2024

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia baada ya kumtembelea na kukagua athari zilizosababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini katika maeneo ya Taweta, Masagati, Utengule na Malinyi katika Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero Mkoani MorogoroAprili 16.2024.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia athari zilizosababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini katika maeneo ya Taweta, Masagati, Utengule na Malinyi katika Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero Mkoani MorogoroAprili 16.2024.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia mkono wananchi wa Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro, wakati alikagua athari zilizosababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini katika maeneo ya Taweta, Masagati, Utengule na MalinyiAprili 16.2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Morogoro Adam Malimawakati alipowasili katika Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro, wakati alikagua athari zilizosababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini katika maeneo ya Taweta, Masagati, Utengule na MalinyiAprili 16.2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia ameridhia kutoa tani 189 za mbegu za mpunga, mahindi na alizeti ili zisambazwe kwa wakulima wa wilaya ya Kilombero.


“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatoa pole kwa wananchi wote walioathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazonyesha nchini, lakini pia ametoa mbegu hizo ili kuhakikisha wale waliopata athari katika mashamba yao waweze kuendelea na shughuli za kilimo pale hali itakapokaa sawa,” amesema.

 

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 16, 2024) wakati akizungumza na wananchi wa maeneo ya Mlimba, Taweta, Masagati wilayani Kilombero, mkoani Morogoro ambako alikwenda kukagua athari za mafuriko.  

 

Waziri Mkuu ambaye pia alikagua bonde la mto Kilombero linalojumuisha wilaya tatu za Kilombero, Ulanga na Malinyi, amesema Rais Samia ameelekeza Serikali iendelee kuwahudumia wananchi wote waliopata athari ikiwemo kuimarisha maeneo ya utoaji huduma za afya, kugawa vyakula na kurejesha miundombinu ikiwemo barabara na reli.

 

“Watanzania tuwe watulivu, Serikali yenu ipo kazini. Rais wetu Dkt. Samia ametupa maelekezo ya kuhakikisha tunawahudumia na kurejesha hali, tutaleta vyakula na tayari madaktari takribani 20 wameshasambazwa kwenye mikoa ya Morogoro na Pwani ili waweke kambi za utoaji huduma za afya.”

 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza TARURA, TANROADS na TAZARA zishirikiane kufanya ukarabati katika maeneo yote yaliyopata athari wakati Serikali inasubiri kumalizika kwa mvua ili iweze kufanya ukarabati mkubwa.

 

Waziri Mkuu anaelekea Ikwiriri, Muhoro na Chumbi wilayani Rufiji, mkoani Pwani ambako atakagua athari za mafuriko na kuwasalimia wananchi.

Posted by MROKI On Tuesday, April 16, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo