Akizungumza mbele ya Mgeni rasmi Mh. Ngurangwa alisisitiza suala la malezi bora ambayo msingi wake ni mafundisho sahihi ya kidini kwa mtoto tangu akiwa na umri mdogo, huku Quran ikiwa ni nyenzo ya kuusimika msingi huo.
Aidha Mgeni rasmi sheikh wa wilaya alisisitiza umuhimu wa kuienzi, na kuikuza quran kwa vijana wadogo ni jambo jema lenye kheri na taathira kubwa kwa jamii.
Pamoja na hayo Mh. Diwani aliwashukuru washiriki wote, walimu, wazazi na walezi lakini kipekee wadau na viongozi mbalimbali waliowezesha kufana kwa mashindano hayo.
Zawadi mbalimbali zimetoelewa kwa watoto waliofanya vizuri zikiwemo TV, BAISKELI, MADAFTARI, MISAHAFU na PESA TASLIMU kwa washindi wa Juzuu 1,2,3 na 5.
0 comments:
Post a Comment