Nafasi Ya Matangazo

April 28, 2024










Kamati ya Uongozi wa Mradi wa Julius Nyerere uliyochini ya Mwenyekiti Mha. Cyprian John Luhemeja ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu Rais Muungano na Mazingira wametembelea Bwawa la kufua umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) katika mto Rufiji kwa lengo la kujionea maendeleo ya Mradi huo ambao unatarajia kuzalisha Megawati 2115 za umeme

Viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti Mha. Cyprian John Luhemeja  wametembelea mradi huo , Aprili 27,2024 ambapo katika ziara hiyo waliambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt. James Mataragio.

Baada ya Kutembelea Bwawa la Julius Nyerere Mha. Cyprian alisema wamefurahishwa na namna wataalamu wa Kitaanzania walivyoweza kusimamia mradi huo kwa ustadi mkubwa.

Aidha Mha. Cyprian amewasisitiza  wataalamu wanaotekeleza mradi huo kuwa watanzania wanahitaji kupata huduma ya umeme wa uhakika

" Najuwa kazi kubwa imefanyika na serikali imewekeza fedha nyingi hivyo watanzania wanatarajia kupata umeme wa uhakika muda si mrefu" alisema Mha.Cyprian

Hivyohivyo Mha. Cyprian Aliwapongeza  Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme ( TANESCO) na wadau wengine kwa kuhakikisha  mradi huo unatekelezwa kwa ufasaha.
Posted by MROKI On Sunday, April 28, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo