Nafasi Ya Matangazo

April 19, 2024








Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Leo Aprili 18, 2024 ameshiriki hafla ya ugawaji wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mundemu wanaosomeshwa na Mfuko wa kusaidia na kuboresha Elimu katika Kata ya Mundemu Wilayani Bahi.

Hafla hiyo ya ugawaji wa magodoro na sare kwa wanafunzi hao, imefuatia Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Bahi kuanzisha mfuko wa kusaidia na kuboresha Elimu kwenye Halmashauri hiyo hasa kwa watoto wanaotoka kwenye familia zenye uhitaji.

Lengo hasa la mfuko huo ni kusaidia wanafunzi kuendelea na masomo kwa kuwafanikishia Mahitaji muhimu yanayohitajika kwa ajili ya Elimu kama vile ada, sare za shule, vifaa pamoja na fedha za kujikimu.

Mkuu wa Mkoa ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuonesha juhudi za kuinua Elimu kwa vitendo.

"Bahi mumeonesha kujitambua, ukiiona Bahi umeona Elimu. Nyinyi mumetafuta utatuzi wa changamoto za Elimu kwani ndio kazi ya Serikali ya awamu ya Sita. Kusomesha watoto 1,036 kwa kuwalipia ada, sare za shule na fedha za kujikimu inawafanya watoto hawa waanze kufurahia masomo na kupenda kwenda shule". Amesema Mhe. Senyamule.

Mbali na hilo, Mhe. Senyamule ametoa maelekezo kwa Halmashauri nyingine za Mkoa wa Dodoma kuiga mfano wa Bahi kwa kuanzisha mifuko ya Elimu ili kusaidia wanafunzi wenye uhitaji kuweza kuendelea na masomo na kutimiza ndoto zao.

Pia ametoa wito wa kuhakikisha wazazi wa watoto wenye uhitaji na sifa za kuwa shuleni wanasaidiwa ili wafike shuleni.

Mfuko wa kusaidia na kuboresha Elimu Halmashauri ya Bahi, ulianzishwa Oktoba 2014 na unasaidia wanafunzi 1,036 umekua na mafanikio kadha wa kadha ikiwemo kumaliza tatizo la wazazi kushawishi watoto kujifelisha, kuongeza ufaulu, kuongeza idadi ya wasomi, kuongeza hamasa ya Elimu, kutoa magodoro 49 kwa wanafunzi wa bweni n.k
Posted by MROKI On Friday, April 19, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo