Kamati ya Siasa ya chama cha mapinduzi Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es Salaam, ikiongozwa na ,Mwenyekiti wa Wilaya ya Kigamboni, CDE. Shabani Sikunjema leo Aprili,16,2024 imefanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara, shule na baadhi ya makazi ya wananchi katika Maeneo mbalimbali yaliyo athiriwa na mvua zinazoendelea katika Kata za Pemba Mnanzi, kibada, Kisarewe II,na Kimbiji.
Aidha kamati ya siasa imemataka Mkurugenzi wa manispaa Ndg. ERASTO Kiwale kuhakikisha maeneo ya shule yanachukuliwa tahadhali kubwa ili kulinda watoto na magonjwa ya mlipuko yanayoweza kusababishwa na kutuama kwa maji ya mvua kwenye maeneo yanayotumiwa na wanafunzi.
Sambamba na hilo katibu wa Chama cha mapinduzi ndugu, Stanley Mkandawile amewataka Tarula na Tanroads kuongeza nguvu kwenye ujenzi wa miradi ya barabara inayoendelea ili kutatua changamoto za ukosefu wa mawasiliano ya baranara Kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment