Nafasi Ya Matangazo

March 06, 2024












🔴Wananchi wengi waguswa na tukio hilo na kupongeza Tume ya Madini 

Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani leo Machi 06, 2024 wanawake kutoka Tume ya Madini wamefanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kulipia gharama za matibabu  kwa wagonjwa wenye uhitaji maalum ikiwemo  vifaa tiba, dawa, operesheni pamoja na kugawa baadhi ya vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuwatia moyo wagonjwa hao.

Akizungumza kwa niaba ya wanawake wa Tume ya Madini, Meneja wa Utawala na Rasilimali Watu, Fatma Chondo amesema kuwa ziara  hiyo ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani itakayofanyika tarehe 08, Machi 2024 ambapo wameamua kuwatembelea wagonjwa wenye uhitaji, kuwapatia msaada na kuwatia moyo.

“Tunatambua kila mtu ana mahitaji mbalimbali lakini nashukuru kwa michango iliyotolewa na Tume ya Madini kufanikisha kulipia baadhi ya gharama kwa wagonjwa 13 ambao wamekuwa wakipatiwa matibabu lakini wamepata changamoto ya kulipia gharama za kutibiwa” amesema Chondo.

Ameendelea kusema kuwa, “ Natoa wito kwa wanawake wengine kuwa sisi kama walezi tunategemewa na tuendelee kuwasaidia watanzania wenzetu wenye mahitaji zaidi lakini wanakosa msaada, ambapo kutoa ni akiba ya baadae pamoja na familia zetu.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Hospitali ya Rufaa ya Dodoma,  Tegemea Jassel ameshukuru wanawake wa Tume ya Madini kwa umoja huo na kusisitiza wanawake wengine kujitokeza ili kuondokana na matatizo yanayowakabili wagonjwa. 

Naye Muuguzi Mfawidhi Msaidizi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa  Dodoma, Mariam Lyimo ameshukuru kwa jitihada zilizofanywa na wanawake na kusisitiza kuendelea kujitokeza katika kuwasaidia wenye mahitaji maalum na walioshindwa kupewa matibabu kama wanawake wa madini.

Mmoja kati ya wagonjwa walionufaika na msaada huo, Daudi Muna ameushukuru uongozi wa Tume ya Madini kwa jambo walilofanya la kuwapatia msaada na kuongeza kuwa imewatia moyo sana na kujiona wa thamani sana katika jamii.
Posted by MROKI On Wednesday, March 06, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo