Nafasi Ya Matangazo

March 11, 2024

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru kwa niaba ya familia  Waumini wa Dini ya Kiislamu sehemu mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar walioandaa Dua na Khitma ya kumwombea Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo katika Khitma na Dua Maalum ya kumwombea  Baba yake mzazi , Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi  iliyoandaliwa na Chama cha Mapinduzi Zanzibar katika Masjid Mushawar Mwembe Shauri Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja tarehe: 11 Machi 2024.

Aidha Rais  Dk.Mwinyi pia amewashukuru wananchi wote walioshiriki katika Dua hizo.

Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wa Serikali, Dini na Vyama vya Siasa wameshiriki Dua na Khitma hiyo.













Posted by MROKI On Monday, March 11, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo