Nafasi Ya Matangazo

March 12, 2024







Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ameongoza Mkutano wa Wabunge wote wa kupokea Mapendekezo ya Serikali ya Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka fedha 2024/2025.Mkutano huo umefanyika leo tarehe 11 Machi, 2024 katika ukumbi wa Pius Msekwa Jijini Dodoma.

Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2024/25 yaliwasilishwa na Waziri wa Ofisi ya Rais-Uwekezaji na Mipango, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo huku Mapendekezo ya Mfumo na   Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka fedha 2024/2025 yakiwasilishwa na  Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba.
 
Mara ya baada ya kuwasilishwa kwa  Mapendekezo hayo, Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu kwa niaba ya Mhe. Spika aliekeza Kamati ya Kudumu ya Bajeti kuyafanyia kazi Mapendekezo hayo na kuzishauri Kamati za kisekta ipasavyo.
 
Kwa upande mwingine Waheshimiwa Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge takribani 14 wataanza kufanya ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo nchi nzima.
Posted by MROKI On Tuesday, March 12, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo