Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na sherehe za Mwaka huu za siku ya wanawake Duaniani zinazoadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka.
Na Mwandishi wetu, Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaaliwa anatafaji kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya mwaka huu ya wanawake Duaniani ngazi ya Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma leo Februari 12,2024, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema Waziri Mkuu atamuwakilisha RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan na maadhimisho hayo yatafanyika Wilaya ya Chamwino Mkoani hapa.
Mhe. Senyamule amesema lengo Kuu la kuadhimisha siku ya wanawake Duniani ni kutoa fursa kwa jamii kupima utekelezaji wa Maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbali mbali za Kimataifa, Kikanda na zinazohusu masuala ya maendeleo ya jinsia na uwekezaji kwa Wanawake.
“Kuadhimisha siku ya wanawake Duniani ni kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutambua na kuthamini uwezo na mchango mkubwa wa wanawake katika kuleta maendeleo pamoja na kuelezea jitihada mbalimbali za Serikali na wadau mbalimbali katika kuwajengea uwezo wanawake.
“Mwaka 2024 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma itaadhimisha siku hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia wanawake na makundi maalum pamoja na Taasisi ya FAGDI. Maadhimisho ya mwaka huu yanatarajiwa kufanyika kwa namna tofauti na miaka mingine na Kimkoa yataadhimishwa katika Wilaya ya Chamwino”. Ameongeza Mhe. Senyamule.
0 comments:
Post a Comment