Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo
amesema Serikali inatarajia kupata wastani wa shilingi
trilioni 2.4 kutokana
na biashara ya kaboni ambazo zitachangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la paifa.
Dkt. Jafo ameliarifu
Bunge leo Februari 5, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Buhigwe Mhe. Kavejuru
Felix aliyetaka kujua biashara
ya kaboni katika misitu ya asili na ya kupanda imechangia kiasi gani kwenye
pato la taifa tangu iingie nchini.
Wamesema
hadi kufikia Desemba 31, 2023 Serikali imepokea jumla ya maombi 35 ya miradi
mbalimbali ya biashara hiyo pindi mchakato wa usajili utakapokamilika na kuanza
kutekelezwa kwa miradi hii.
“Katika
miaka ya hivi karibuni kumeibuka soko huria la biashara ya kaboni ikijumuisha misitu
ya asili na ya kupanda na imeanza kushamiri hapa nchini na kuonesha inaweza
kuchangia kwenye pato la taifa,” alisema Dkt. Jafo.
Halikadhalika,
Waziri Jafo alisema katika kipindi cha mwaka 2018-22 fedha zilizopokelewa
kupitia miradi inayotekelezwa kwenye halmashauri mbalimbali hapa nchini
inafikia shilingi bilioni 32.
Akiendelea
kujibu maswali ya nyongeza kuhusu mkakati wa utoaji elimu ya biashara hiyo,
Dkt. Jafo alisema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa
kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEM pamoja na Wizara ya Maliasili na Utali imefanya
mkutano na wakuu wa mikoa na wilaya kupeleka ujumbe.
Aliongeza
kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea kutoa elimu kwa wananchi na
kuwahamasisha kupanda miti kwa wingi ili kunufaika na biashara hiyo na
kuhifadhi mazingira.
Pamoja
na hayo, Waziri Jafo alisema pia Tanzania imetumia fursa ya ushiriki katika
Mkutano wa 28 Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Dubai, Falme za Kiarabu
kutangaza biashara ya kaboni.
Kutokana na hatua hiyo alisema kuwa mwitikio wa wananchi na kampuni za
ndani na nje kushiriki katika biashara ya kaboni umekuwa mkubwa hivyo kuongeza pato
la taifa.
Hivyo,
Waziri Jafo alitumia nafasi hiyo kuwasihi wabunge katika maeneo yao
yaliyobarikiwa kuwa na misitu kuona kuwa ni muhimu kushiriki katika biashara
hiyo ili si kuongeza pato la taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)






0 comments:
Post a Comment