Mbunge wa Lupa, mhe. Masache Njelu Kasaka akiuliza swali Bungeni Jijini Dodoma leo ambapo alitaka kujua ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Makongolosi – Rungwa.
************
Serikali imesema inajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Mbeya -
Chunya - Makongolosi - Rungwa - Mkiwa (km 503.36) kwa awamu ambapo sehemu ya
Mbeya - Chunya - Makongolosi (km 111) ujenzi umekamilika.Hayo yamesemwa Bungeni Jijini Dodoma leo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mha. Godfrey M. Kasekenya wakati akijibu swali
la Mbunge wa Lupa, mhe. Masache Njelu Kasaka aliyetaka kujua ni lini Serikali
itaanza ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Makongolosi – Rungwa.
Aidha Mha. Kasekenya ameliambia Bunge kuwa Ujenzi wa sehemu ya Noranga -
Itigi - Mkiwa (km 56.9) sehemu ya Noranga - Itigi (Mlongaji) (km 25.) umefikia
asilimia 72.
Sehemu ya Noranga - Doroto (km 6) na Itigi - Mkiwa (km 25.6) kazi ya
ujenzi zimeanza na utekelezaji wa mradi unaendelea.
Kwa sehemu iliyobaki ya barabara ya Makongolosi - Rungwa – Noranga (km
356) Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi.







0 comments:
Post a Comment