Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza leo wakati wa kufungua mafunzo ya siku tatu ya watendaji wa uchaguzi katika uchaguzi mdogo wa Kata 23 unaotaraji kufanyika Machi 20,2024. Mafunzo hayo ya watendaji wa uchaguzi yanayofanyika Mkoani Morogoro.
Watendaji wa uchaguzi wanaohudhuria mafunzo ya siku tatu yaliyoanza leo Februari 20,2024 hadi Februari 23,2024 wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi aliyekua akifungua mafunzo hayo Mkoani Morogoro.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe. Aisha Hassan Waziri akiwaapisha watendaji wa Uchaguzi watakaoshiriki katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani wa Kata 23 za Tanzania bara. Watendaji hao wamekula kiapo cha kutunza Siri na kujitoa uanchama wakati wa mafunzo yao ya siku tatu yanayofanyika Mkoani Morogoro kuanzia leo Februari 20 hadi 23,2024.
Watendaji wa Uchaguzi watakaoshiriki katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani wa Kata 23 za Tanzania bara wakila kiapo cha kutunza Siri na kujitoa uanchama wakati wa mafunzo yao ya siku tatu yanayofanyika Mkoani Morogoro kuanzia leo Februari 20 hadi 23,2024.

************
Na
Mwandishi wetu, MorogoroWatendaji
wa uchaguzi kwenye uchaguzi mdogo wa kata 23 za Tanzania Bara uliotangazwa hivi
karibuni na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wametakiwa kuwashirikisha kwa ukaribu
wadau wa uchaguzi kwenye maeneo yao.
Wito
huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa)
Jacobs Mwambegele leo Februari 20, 2024
wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi yanayofanyika Mkoani
Morogoro.
Uchaguzi
huo utafanyika Machi 20, 2024 ambapo fomu
za uteuzi zitatolewa kuanzia Februari 27,
2024 hadi Machi 4, 2024, uteuzi wa wagombea utafanyika Machi 4, 2024 na kampeni
za uchaguzi zitafanyika kuanzia Machi 5 hadi 19, 2024.
“Napenda
niwakumbushe na kuwasisitiza kuwa, wakati wote wa mchakato wa uchaguzi , ni
vema mkavishirikisha kwa karibu vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi
katika maeneo yenu kuhusu masuala ya kiuchaguzi ambayo wanastahili
kushirikishwa kwani jambo hilo litawarahisishia
utekelezaji wa majukumu yenu,” amesema Jaji Mwambegele.
Pia,
amekumbusha juu ya umuhimu wa kuvipatia vyama vya siasa orodha ya vituo vya
kupigia kura ili kuviwezesha kupanga mawakala.
Ameongeza
kuwa ni muhimu kwa watendaji hao wa uchaguzi, kuhakikisha wanayatambua na
kuyajua vyema maeneo ambayo uchaguzi
utaendeshwa ikiwemo miundombinu ya kufika katika kata na vituo vya kupigia
kura.
Jaji
Mwambegele alisisitiza kuhusu umuhimu wa kufanya utambuzi na kukagua vituo vya kupigia kura mapema ili kubaini
mahitaji maalum ya vituo husika kwa lengo la
kuhakikisha mpangilio mzuri ambao utaruhusu uchaguzi kufanyika kwa
utulivu na amani.
Mwenyekiti
huyo wa Tume amekumbusha juu ya wajibu wa kuhakikisha kwamba watendaji wa vituo
watakao ajiriwa wanakuwa watu wenye weledi na wanaojitambua.
“Tuachane
na upendeleo kwa ndugu na jamaa ambao hawana sifa za kufanya shughuli za
uchaguzi,” amesema Jaji Mwambegele.
“Mhakikishe siku ya uchaguzi mnaweka utaratibu
utakaowezesha kila kituo cha kupigia kura kinafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufanya
mawasiliano na Tume pale ambapo utahitajika ushauri kuhusiana na masuala ya
uchaguzi,” Jaji Mwambegele aliwasisitiza watendaji hao.
Aliwakumbusha
kuwa uchaguzi ni jambo la kisheria na kwamba sheria na taratibu zikifuatwa ndio
msingi wa uchaguzi kuwa mzuri, wenye ufanisi na hivyo kupunguza kama siyo
kuondoa kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.
“Nachukua
nafasi hii kuwaasa kuwa pamoja na uzoefu ambao baadhi yenu mnao katika
uendeshaji wa uchaguzi, mhakikishe
mnazingatia maelekezo mtakayopewa na Tume badala ya kufanya kazi kwa mazoea.
Hata kama umeshasimamia chaguzi kadhaa hapo nyuma, lakini uchaguzi huu mdogo
unaojumuisha kata 23 haujawahi kuusimamia,” amesema.
Kata
zitakazofanya uchaguzi huo mdogo ni Kimbiji (Halmashauri ya Manispaa ya
Kigamboni), Kasingirima (Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji), Ndevelwa
(Halmashauri ya Manispaa ya Tabora), Msangani (Halmashauri ya Mji Kibaha),
Fukayosi (Halmashauri ya Wilaya ya
Bagamoyo), Mlanzi (Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti), Utiri (Halmashauri ya Mji
Mbinga) na Mbingamhalule (Halmashauri ya Wilaya ya Songea).
Nyingine
ni Isebya (Halmashauri ya Wilaya ya
Mbogwe), Kibata (Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa), Mshikamano (Halmashauri ya Wilaya ya Musoma), Busegwe
(Halmashauri ya Wilaya ya Butiama), Nkokwa (Halmashauri ya Wilaya ya Kyela),
Kamwene (Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba), Chipuputa (Halmashauri ya Wilaya ya
Nanyumbu), Buzilasoga (Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema), Mhande (Halmashauri
ya Wilaya ya Kwimba), Kabwe (Halmashauri ya Nkasi), Bukundi (Halmashauri ya
Wilaya ya Meatu) Mkuzi (Halmashauri ya Wilaya ya Muheza) na Boma, Mtimbwani na
Mayomboni (Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga).
0 comments:
Post a Comment