Nafasi Ya Matangazo

February 16, 2024






Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amefanya ziara ya kikazi yenye  lengo la kukagua miradi ya kimaendeleo kwenye shule ya msingi Makulu pamoja na Hospital ya Wilaya ya Dodoma leo tarehe 15 Februari, 2024.
 
Katika shule ya Msingi Makulu, amekagua mradi wa ujenzi wa vyumba Vitano vya madarasa, ofisi 2 za walimu uliogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 100 na ujenzi wa matundu ya vyoo 12 kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wasichana na wavulana pamoja na vyoo vya walimu walimu kwa gharama ya shilingi Milioni 204, fedha kutoka Serikali kuu.

Mhe. Senyamule amesema kila Halmashauri za Wilaya zihakikishe zinaaza ujenzi katika fedha zilizoigia mwezi Disemba kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya elimu na afya.

“Kila  mradi ni lazima ukamilike kwa wakati uliopagwa na isitokee sababu yoyote ya kukwamisha miradi hiyo. Hatupo tayari kuona kuna watu bado wanakwamisha miradi iliyoletwa na Serikali yetu inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan.

“Lengo la miradi hii kuletwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyo bora na kwa wakati ndio maana amekuwa kinara katika kuhakikisha anawezesha Miradi ya Elimu na Afya” Mhe. Senyamule.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma Dk.Andrew Method amesema Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 ambazo zinajenga Jengo la Mama na mtoto, Maabara na Idara ya Magonjwa ya nje. Pia  imepokea shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa kichomea taka, Jengo la Mionzi na Duka la Dawa ambalo ujenzi wake umefikia 38%
Posted by MROKI On Friday, February 16, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo