Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Imeelezwa kuwa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la mto Ruaha Mkuu lililopo kwenye barabara ya Kidatu – Ifakara lenye urefu wa mita 133 mkoani Morogoro, utakapokamilika utakuwa na manufaa makubwa ikiwemo kuchagiza maendeleo, kukuza uchumi pamoja na kuunganisha mkoa huo na Mikoa mingine ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Lindi na Mtwara na nchi jirani.
Akizungumza hivi karibuni Kaimu
Mhandisi Mkazi wa Mradi huo unaokwenda sambamba na ujenzi wa barabara hiyo
yenye urefu wa kilometa 66.9 kiwango cha lami, Mhandisi Marcel Kiimu amesema
katika daraja hilo magari yatapita mawili ikiwa ni moja kila upande, tofauti na
awali yalipita moja kwani ni jembamba hivyo limesababisha msongamano wa magari.
Amesema pia kwenye barabara
hiyo kumejengwa kumejengwa madaraja mengine ya kawaida manne ambayo ni Ikela,
Msolwa, Sumbugulu na Kisawasawa, makalavati makubwa 45 yenye urefu wa mita 584
kwa kila moja na makalvati ya kawaida 249, ambayo yote yatasaidia kupitisha
maji kwa haraka.
Mradi huo wa kimkakati ni
sehemu ya mkakati wa Taifa wa kuwasaidia wakulima wadogo wanaolima mazao ya
chakula na biashara kupitia Programu ya uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa
Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), waliopo katika Bonde la Mto Kilombero, Ulanga,
Mlimba na Malinyi.
Amesema barabara hiyo itakuwa
na upana wa mita 9.5 ikiwa ni njia ya magari yenye upana wa mita 6.5 yenye lami
nzito (asphalt concrete) na mabega ya barabara yenye upana wa mita 1.5 kwa kila
upande wa maeneo yasiyokuwa na miji na upana wa mita 2.0 kila upande wenye
miji, mitaro ya kupitisha maji na vivuko vya watembea kwa miguu.
Mha. Kiimu ameongeza kuwa mradi
huo ujenzi wa barabara ya Kidatu-
Ifakara unaotarajiwa kukamilika Machi 2024 unasimamiwa na Kitengo cha TECU cha
Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), ambapo utatumia gharama ya zaidi ya Shilingi
Bil. 128.15, unawafanyakazi 792 kati yao wazawa ni 779 na 13 ni wageni,
miongoni mwao wanaume ni 703 na wanawake ni 89. Pia kuna wahandisi wahitimu wa
vyuo vikuu watano na wanafunzi toka vyuo vikuu saba.
Imeelezwa kuwa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la mto Ruaha Mkuu lililopo kwenye barabara ya Kidatu – Ifakara lenye urefu wa mita 133 mkoani Morogoro, utakapokamilika utakuwa na manufaa makubwa ikiwemo kuchagiza maendeleo, kukuza uchumi pamoja na kuunganisha mkoa huo na Mikoa mingine ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Lindi na Mtwara na nchi jirani.
0 comments:
Post a Comment