Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, leo tarehe 21 Novemba 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Singapore aliyefika Ofisini kwake kwenye Jengo la Mkapa Jijini Dodoma lengo la ujio huo likiwa ni kukuza ushirikiano kati ya Singapore na Tanzania hususani katika Mkoa wa Dodoma.
Ujumbe huo unadhamira ya kuwekeza katika Sekta mbalimbali zikiwemo ikiwemo miundombinu, fursa za masomo na Ushirikiano wa kujengeana uwezo katika kukuza Jiji la Dodoma
Aidha, ujumbe huo umeongozwa na Bw.Douglas Foo, Balozi wa Tanzania nchini Singapore na Bi. LEE Zhu'ai Sian, Mkurugenzi Msaidizi, Wizara ya Mambo ya Nje Singapore.
0 comments:
Post a Comment