Nafasi Ya Matangazo

October 11, 2023

Wachezaji Sharifa (kushoto) wa Wizara ya Uchukuzi na Christa Njovu  wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakichuana katika mchezo wa bao  wa Shirikisho la michezo ya wizara na Idara za serikali Tanzania (SHIMIWI) uliofanyika kwenye Chuo cha Kikatoliki Ruaha mkoani Iringa.Jenny aliibuka mshindi wa tatu.
Wachezaji Zuhura Mtola wa Wizara ya Ujenzi na Jenny Mkomwa wa RAS Ruvuma wakiusoma mchezo wa bao kabla ya kuanza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kwa upande wa wanaume wa Shirikisho la michezo ya wizara na Idara za serikali Tanzania (SHIMIWI) uliofanyika kwenye Chuo cha Kikatoliki Ruaha mkoani Iringa.Jenny aliibuka mshindi wa tatu.
Mchezaji  Wizara ya Kilimo (kulia) akicheza kete dhidi ya Adam Ramadhani wa Wizara ya Mambo ya Ndani katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kwa wanaume wa Shirikisho la michezo ya wizara na Idara za serikali Tanzania (SHIMIWI) uliofanyika kwenye Chuo cha Kikatoliki Ruaha mkoani Iringa.Mtipe aliibuka mshindi wa tatu.
Bingwa wa mchezo wa bao kwa Wanawake, Sarafia Hokororo RAS Lindi (kulia) akicheza dhidi ya Rebecca Mwakaje wa Mahakama katika mchezo wa fainali wa bao wa shirikisho la michezo ya wizara na Idara za serikali Tanzania (SHIMIWI) uliofanyika kwenye Chuo cha Kikatoliki Ruaha mkoani Iringa.
Mchezaji Aden Michael wa Wizara ya Ujenzi (kulia) akicheza dhidi ya Hashim Mtomondela wa Mahakama katika mchezo wa fainali wa bao katika michezo ya shirikisho la michezo ya wizara na Idara za serikali Tanzania (SHIMIWI) uliofanyika kwenye Chuo cha Kikatoliki Ruaha mkoani Iringa. Aden ametwaa ubingwa.
***********
Na Mwandishi Wetu, Iringa
WAZAZI wameshauriwa kuwafundisha Watoto wao kucheza mchezo wa bao kwa kuwa litawachangamsha na kuwajenga kiakili.
Kauli hiyo imetolewa na bingwa wa mchezo huo, Aden Michael wa Wizara ya Ujenzi katika michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI), inayoendelea kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa, Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha na Samora.
Michael amesema kuwa Watanzania wote waienzi michezo ya jadi ikiwemo bao kwa kuwafundisha Watoto ili iendelee kuwepo. 
“Huu ni mchezo mzuri kwani ukiuangalia utadhani watu wanaocheza ni wazembe na hawapendi kufanya kazi, huu ni mchezo mzuri mtu anaweza kucheza hata baada ya kufanya kazi, unafikirisha akili na kutumia sana hesabu,” amesema Michael.
Katika hatua nyingine mshindi wa pili kwa wanaume, Hashimu Mtomondela amesema mchezo wa bao kwa mwaka huu umekuwa na ushindani mkubwa kutokana na washiriki kujiandaa vyema.
Mtomondela amesema kuwa ushindani huo umeonekana kuanzia hatua ya makundi, 16 bora, nane bora, nusu fainali na fainali, ambapo kila mchezo ulilazimu kufanyika mitatu baada ya michezo ya kwanza na pili kutoka sare ya pointi moja kila mshiriki mmoja.
“Kila mchezaji aliyeshiriki alikuwa amepania na kufanya mchezo kuwa na msisimko na mshindi amepatikana kihalali kabisa ukiangalia mimi mwenyewe mwaka jana nilishika nafasi ya tatu, lakini mwaka huu nimekuwa wa pili,” amesema Mtomondela.
Ametoa ushauri washiriki wote wasibweteke baada ya kumaliza mashindano waendelee kucheza warudipo majumbani na kutumia mapumziko ya mwishoni mwa juma.
Kwa upande wa wanawake ubingwa wa mchezo huo wa bao umechukuliwa na Sarafia Hokororo wa RAS Lindi aliyemshinda Rebecca Mwakaje wa Mahakama kwa alama 2-1; huku ushindi wa tatu umechukuliwa na Jenny Mkomwa wa RAS Ruvuma aliyemshinda Zuhura Mtola wa Wizara ya Ujenzi. Mshindi wa tatu kwa wanaume umechukuliwa na Nyagalu Mtipe wa Wizara ya Kilimo aliyemfunga Adam Ramadhani wa Wizara ya Mambo ya Ndani.
Posted by MROKI On Wednesday, October 11, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo