Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ukata wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake kikazi wilayani humo tarehe 10 Oktoba, 2023.Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga akisalimiana na wanafunzi wa shule ya msingi Ukata wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo tarehe 10 Oktoba, 2023.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga akiwasha umeme kwa mara ya kwanza katika Zahanati ya Lundomato Kijiji cha Ukata Mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake kikazi wilayani humo tarehe 10 Oktoba, 2023.
Mhe. Kapinga amesema hayo wakati wa hafla ya
kuwasha umeme kwa mara ya kwanza katika Kijiji cha Ukata wilayani Mbinga wakati
wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Usambazaji wa umeme Vijijini Awamu ya
Tatu Mzunguko wa pili Mkoani Ruvuma tarehe 10 Oktoba, 2023.
Amefafanua kwamba nia ya Serikali ni
kuhakikisha mazingira ya ufundishaji na pamoja na ya kusomea kwa watoto wote
nchini yanaimarishwa, pia wazazi wanasomesha watoto kwa jasho kwa mategemeo ya
kupata viongozi bora wa kesho.
“Lengo la Serikali ni kuhakikisha tunaboresha
mazingira ya ufundishaji ili walimu waweze kutumia vitendea kazi vinavyoendana na ulimwengu wa Sayansi na
Teknolojia, haiwezekani mwalimu asiwe na Kompyuta wala na Printer akiwa
anafundisha ili kusaidia mtoto tutakuwa tunalea taifa la aina gani? Kwahiyo ni
lazima kuweka umeme sababu Dunia nzima inaenda na maendeleo ya sayansi na
teknolojia” Alisisitiza Mhe. Kapinga.
Mhe. Kapinga aliwaeleza wananchi kuwa
maendeleo ni hatua hivyo mradi wa REA
unatekelezwa kwa awamu katika vijiji vyote nchini, na ifikapo Desemba 2023
vijiji vyote vitaunganishwa na umeme na kama kuna kitakachosalia kitaunganishwa
wakati wa kuunganisha vijiji 22024.
Katika ziara hiyo Mhe. Kapinga aliambatana na
Viongozi kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO).
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga akiwasha umeme kwa mara ya kwanza katika Zahanati ya Lundomato Kijiji cha Ukata Mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake kikazi wilayani humo tarehe 10 Oktoba, 2023.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga akipanda mti katika Shule ya Sekondari Mkinga wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake kikazi wilayani humo tarehe 10 Oktoba, 2023.
**************
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga,
amesema upatikanaji wa Umeme Vijijini kunaimarisha ubora wa elimu kwa shule za
Msingi na Sekondari nchini.





0 comments:
Post a Comment