Kipa wa timu ya RAS Simiyu Ally Mzee (jezi ya njano) akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na Mustafa Khalfan wa Maendeleo ya Jamii akifunga bao la pili kwa timu yake katika michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) uliofanyika leo kwenye uwanja wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa mkoani Iringa. Maendeleo ya Jamii wameshinda mabao 2-0.
Timu ya wanaume ya Ofisi ya Rais Ikulu (kushoto) wakiwavutawizara ya Maliasili na Utalii kwa mivuto 2-0 katika mchezo wa michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) uliofanyika leo kwenye uwanja wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa.
Timu ya wanawake ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo (kulia) wakivutwa na timu ya OIfisi ya Bunge kwa mivuto 2-0 katika mchezo wa michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) uliofanyika leo kwenye uwanja wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa.
Mchezaji Anna Mrisho (WA) wat imu ya Wakala ya Barabara Vijijini (TARURA) akiwania mpira pamoja na Martha Kibona (CD) wa Wizara ya Uchukuzi katika mchezo wa netiboli wa michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) uliofanyika leo kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (RUCU) mkoani Iringa. Uchukuzi wameshinda kwa magoli 24-5.
TIMU mbalimbali za mchezo wa mpira wa miguu zinazoshiriki kwenye michezo ya Shirikisho la michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI), inayofanyika kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa na Samora mkoani hapa zimeonesha kandanda safi na kufanya zishangiliwe na mashabiki.
Timu hizo zinazoundwa na wachezaji wengi vijana ukiacha wakongwe wachache, zimeleta burudani kwa mashabiki wanaofika kutazama michezo hii ambayo ilianza tarehe 29 Septemba, 2023 na inatarajia kufikia kilele Oktoba 14, 2023; ambapo timu ya ya Maendeleo ya Jamii iliwafunga Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa magoli 2-0, yaliyofungwa na Muhidin Gahatano na Mustafa Khalfan.
Katika mchezo mwingine timu ya Bohari ya Kuu ya Madawa Tanzania (MSD) ilitoshana nguvu na timu ya Waziri Mkuu Sera kwa kufungana magoli 2-2; nayo Wizara ya Mifugo na Uvuvi walitoka sare na TAKUKURU kwa bao 1-1; wakati Wizara ya Uchukuzi walitoka suluhu dhidi ya RAS Mbeya.
Nayo timu ya Katiba na Sheria iliwazamisha RAS Kilimanjaro kwa magoli 7-0; huku Wizara ya Elimu wakiwafunga Wakili Mkuu magoli 2-0; na Wizara ya Ardhi ikipata kipigo kutoka kwa TARURA cha bao 1-0.
Katika mchezo wa netiboli uliochezwa kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (RUCU), timu ya Ukaguzi waliwakagua TAKUKURU kwa kuwafunga magoli 71-8; wakati Wizara ya Uchukuzi wakiwachukua TARURA kwa magoli 24-5; nayo RAS Dar es Salaam waliwaadabisha BRELA kwa kuwafunga magoli 24-13; huku TAMISEMI wakiwafundisha Mashtaka kwa magoli 23-8; wakati MSD wakiwashinda wenyeji RAS Iringa kwa magoli 31-17; timu ya Sheria waliwaliza RAS Lindi kwa magoli 19-12; na Wizara ya Mawasiliano waliwachapa Mambo ya Nje kwa magoli 35-17.
Mechi nyingine timu ya GST ilifungwa na Afya magoli 25-12; huku Utumishi wakiwachapa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa magoli 28-21; na RAS Mwanza waliwashinda Haki kwa 29-18.
Katika michezo ya kamba iliyofanyika kwenye uwanja wa Mkwawa kwa upande wa wanawake timu ya Tume ya Utumishi (1) vs Waziri Mkuu Kazi (1); NEC (0) v Mahakama (2); Viwanda na Biashara (0) vs Mawasiliano (1); Tume ya Madini (1) vs Wizara ya Maji (1); Bunge (2) vs Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo (0); Wizara ya Ujenzi (0) vs Wizara ya Maliasili na Utalii (2); tume ya Sheria (1) vs RAS Shinyanga (1);
Matokeo mengine ni Wizara ya Uchukuzi (2) vs Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi (0); Wizara ya Kilimo (0) vs Hazina (1); Wakili Mkuu (0) vs Wizara ya Mambo ya Nje (2); TAMISEMI (2) vs Mashtaka (0); Waziri Mkuu Sera (2) vs Wizara ya Mambo ya Ndani (0); Wizara ya Afya (2) vs RAS Kigoma (0); RAS Tanga (0) vs Wizara ya Mifugo na Uvuvi (1); Sheria (0) vs RAS Iringa (2).
Kwa upande wa wanaume timu ya Mawasiliano (2) vs Wizara ya Ardhi (0); RAS Kigoma (0) vs TAKUKURU (2); Wizara ya Mambo ya Ndani (2) vs Bohari Kuu ya Madawa (0); Maadili (0) vs Wizara ya Kilimo (2); Wizara ya Ujenzi (0) vs Bunge (1); Wizara ya Maji (2) vs Wakili Mkuu (0); Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo (1) vs Mashtaka (0).
Michezo mingine Sheria (2) vs RAS Simiyu (0); Wizara ya Uchukuzi (1) vs Wizara ya Viwand ana Biashara (0); RAS Shinyanga (1) vs Tume ya Sheria (1); RAS Tanga (0) vs Wizara ya Mifugo na Uvuvi (2); Haki (0) vs NEC (2); Wizara ya Maliasili na Utalii (0) VS Ofisi ya Rais Ikulu (2); na Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania (TSC) ilifuitiwa mchezo wake dhidi ya RAS Lindi baada kukiuka sheria ya kushika kitambaa chekundu wakati mchezaji wa mbele akivuta kamba.









0 comments:
Post a Comment