Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala bora Ndg.Ridhiwani Kikwete amefanya ziara na kuongea na wananchi wa maeneo mbalimbali katika kata ya Talawanda kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo katika Halmashauri ya Chalinze.
Katika ziara hiyo ya Mbunge ambayo ilimfiksha katika vijiji vya Msigi, Magulumatari na Mindukene inalenga zaidi kutoa mrejesho wa kazi kwa wananchi wa maeneo hayo pamoja pia na kutekeleza ahadi waliahidiwa wananchi katika mikutano na maombi mbalimbali. Katika ziara hiyo Mbunge alitekeleza ahadi yake ya kuchangia mabati kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Chama katika kata hiyo.











0 comments:
Post a Comment