Nafasi Ya Matangazo

July 15, 2023

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Kata ya Dunda, Kijiji cha Dunda katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Sehemu ya wananchi na walengwa wa TASAF wa Kata ya Dunda, Kijiji cha Dunda, Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati akizungumza nao alipokuwa kwenye ziara ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika halmashauri hiyo.
Mlengwa wa TASAF, Bi. Mwanaheri Maulidi akitoa ushuhuda kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete namna TASAF ilivyomsaidia kuinua maisha yake wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitazama baadhi ya bidhaa za walengwa wa TASAF katika Kata ya Dunda, Kijiji cha Dunda, Wilaya ya Bagamoyo wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bw. Shauri Selenda akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kuzungumza na wanachi na walengwa wa TASAF wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
**********
Wanufaika wa mradi wa kusaidia kuondoka kaya katika umasikini wamesema, TASAF ni mkombozi wa kweli katika mapambano haya.

 “Tulikuwa hatuna hata hela ya kula lakini leo tumewezeshwa tuna hadi Boti za kufanya uvuvi,”  alisema Mwanaheri Maulidi Mnufaika wa mradi wa TASAF. 

Akizungumza na hadhara iliyojitokeza, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete ameishukuru  na kuipongeza Halmashauri ya Bagamoyo kwa kuunga mkono juhudi hizo kwa kuwakopesha wanufaika wa mradi mkopo katika zile asilimia 10 zilizowezesha kuwatoa katika umaskini.

Bagamoyo ni moja kati ya Halmashauri ambazo , ukombozi wa kaya maskini umefanikiwa sana. Watu wameondoka katika mazingira magumu na sasa wamejenga uwezo kiuchumi na hali zao zinakwenda vizuri. “… ushirikiano mkubwa tuliouona ni mfano wa kuigwa. Hii ni hadithi nzuri inayofaa kuigwa.”

Posted by MROKI On Saturday, July 15, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo