Nafasi Ya Matangazo

July 20, 2023

Wanafunzi wa shule za msingi za Majengo na Magereza katika picha ya pamoja wakiwasikiliza mkuu wa mkoa wa Tabora
Mkuu wa mkoa wa Tabora  Balozi Dkt. Batilda Buriani aliishukuru benki ya NMB  baada ya kupokea  msaada wa vifaa vya shule nne za sekondari 2 na msingi 2.
Meneja wa  NMB kanda ya magharibi  Seka Urio wakati akizungumza mra baada ya kukabidhi msaada wa madwati kwa mkuu wa mkoa wa Tabora .
Mkuu wa wilaya ya Tabora Louis Bula  akitoa neon wakati akipokea msadaa wa madawati viti na meza kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu manispaa ya Tabora.
*************
Na Lucas Raphael,,Tabora
Katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha sekta ya elimu Benki ya NMB kanda ya Magharibi imetoa madawati meza na viti katika shule mbili za Msingi na Mbili za sekondari.
 
Msaada  huo wa madawati 150,Meza 100  na Viti 100 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 25 uliotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya shule ya Msingi Majengo,Magereza na shule za sekondari za Kazima na Lwanzari zote za Mjini Tabora
 
Akizungumza meneja wa  NMB kanda ya magharibi  Seka Urio wakati wakukabidhi msaada huo amesema kufanya hivyo umekuwa niuratibu wakawaida katika kuunga mkono juhudi ya serikali katika kuboresha mazingira ya sekta ya elimu. 

Akipokea madawati hayo mkuu wa mkoa wa Tabora  Balozi Dkt. Batilda Buriani aliishukuru benki ya NMB kwa msaada huo huku akitaja serikali inaendelea na juhudi ya kuhakikisha inamaliza kabisa changamoto ya upungufu wa madawati katika shule za mkoa wa Tabora.

Awali akizungumza mkuu wa wilaya ya Tabora Louis Bula  alisema kwa upande wa wilaya ya Tabora  kuna upungufu wa madawati  8000  huku akitaja msaada huo umekuja katika wakati mahusi wakati serikali ikiendelea kuchukua hatua za makusudi katika kukabiliana na upungufu huo wa madawati.

Baadhi ya wanafunzi walisema msaada huo unakwendak uchangia kwa kiwango kikubwa kuwainua kitaaluma kwani wengi wao wamekuwa wakikaa kwa kubanana madarasani hatua ambayo waimetaja hata walimu imekuwa ikiwapa ugumu katika zoezi  la ufundishaji.

Posted by MROKI On Thursday, July 20, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo