MAMLAKA ya Mapato ( TRA) inatarajia kuanza kutekeleza Sheria ya Bunge ya kuwataka Kila mtanzania aliyefikisha umri wa miaka 18 na kuendelea kuwa na tin namba inayotambulika Kwa jina lake Ili iweze kumsaidia pindi anapotaka kuanzisha biashara.
Bunge la 2022 lilipitisha Sheria ambayo inamtaka kila mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea anapaswa kuwa na tin namba itakayomtambulisha Kwa jina lake.
Uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuondoa vitambulisho vya machinga na bunge kupitisha sheria ya Kila mtanzania kuwa na tin namba.
Akizungumza katika mafunzo ya wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar Es Salaam (DCPC) yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam, Mkurugenzi wa Elimu Kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo amesema kuwa, sheria hiyo inatakiwa kuanza kutekeleza ifikapo Desemba Mwaka huu.
Amesema kuwa tin namba ni muhimu kwa sababu inmtambulisha mtanzania hata kama hana biashara au shughuli ya kufanya.
" Ikiwa utakua na Tin namba Yako itakusaidia wewe mtanzania kukutambulisha hata kama hauna biashara itaandikwa 'Nil' na wale wenye biashara itawasaidia kulipa Kodi kutokana na utambulisho wao wa Haina ya biashara," amesema Kayombo.
Ameongeza kuwa, Sheria hiyo itaanza kutumika Desemba Mwaka huu ambapo mtanzania asiye na tin namba atakua ametenda kosa la jinai na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua zaidi.
Akizungunzia kuhusu utoaji wa leseni za kibiashara, Kayombo amesema kuwa, kuna baadhi ya wafanyabiashara wana tabia ya kukwepa kodi kwa kutumia leseni moja kwenye biashara zaidi ya moja ambazo zote anazimiliki, jambo ambalo ni kinyume na sheria.
Amesema kuwa kitendo hicho ni ukwepaji wa kodi kwa sababu unasababisha Serikali kukosa mapato.
" Unakuta mtu mmoja anamiliki biashara za aina tofauti zaidi ya tatu halafu zipo maeneo tofauti lakini anatumia leseni Moja anachokifanya ni kutoa kivuli (Copy) anabandika kwenye maduka yake hilo ni kosa kisheria, kila biashara inapaswa kuwa na leseni yake, tukikugundua tutakupa elimu lakini ukikahidi tutakuchukulia hatua za kisheria," amesema.
Ameongeza kuwa, hivyo basi kila mtanzania ana wajibu wa kulipa kodi Ili fedha hizo ziweze kurahisisha shughuli za Maendeleo.
" Barabara zinajengwa Kwa sababu wananchi wanalipa kodi, miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa sababu ya Kodi, hivyo basi ni mmoja anapaswa kujua kuwa, kulipa kodi ni muhimu maendeleo ya Taifa," amesema.
Amesema kuwa, Serikali kupitia TRA itaendelea kutoa elimu kwa wananchi Ili waweze kuona umuhimu wa kulipa Kodi.







0 comments:
Post a Comment