Nafasi Ya Matangazo

June 13, 2023


Mhandisi Rogatus Hussein Mativila 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewateua viongozi mbalimbali ambapo amemteua Mhandisi Rogatus Hussein Mativila (pichani) kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Miundombinu).  Mhandisi Mativila alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
 
Aidha Rais Samia amemteua Mhandisi Mohamed Besta kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).  Mhandisi Besta ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (CASSOA).
 
Mhandisi Besta anachukua nafasi ya Mhandisi Rogatus Hussein Mativila ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu.
 
Pia amemteua Kamishna Benedict Wakulyamba kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii. 
 
Kamishna Wakulyamba anachukua nafasi ya Bw. Anderson Mutatembwa ambaye amehamishiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu); na
 
Katika uteuzi mwingine, Rais Samia amemteua Mhandisi Amin Nathaniel Mcharo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
 
Uteuzi huu umeanza tarehe 12 Juni, 2023. 
Posted by MROKI On Tuesday, June 13, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo