Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akikagua Ramani ya Mfumo wa Maji Taka katika Mji wa Serikali Mtumba wakati wa ziara yake aliyoifanya ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mnara wa Mashujaa Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (kulia) akiwa na Mratibu wa Kamati ya zoezi la Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshack Bandawe wakikagua Eneo la mradi wa Ujenzi wa Mnara wa Mashujaa Mtumba Dodoma.
Mhandisi Evance Antony kutoka SUMA JKT akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya Ujenzi wa Mnara wa Mashujaa.*****************
Na Mwandishi wetu- DodomKATIBU MKUU Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya
Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amepongeza maendeleo ya ujenzi wa Uwanja
wa Mashujaa unaojengwa katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Dkt. Yonazi ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua ujenzi huo ambapo ameeleza kwamba unaendelea vizuri na unatarajiwa kukamilika mapema kabla ya Julai 25 mwaka huu ili uweze kutumika kwa ajili ya shughuli za Mashujaa.





0 comments:
Post a Comment