Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe.
Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za
rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima kutokana na vifo vya watu wawili katika ajali ya ndege.
Ajali hiyo imetokea leo saa 5:30 asubuhi katika kiwanja cha ndege cha Matambwe kwenye
Hifadhi ya Taifa ya Nyerere mkoani humo na kusababisha vifo vya watu wawili na
majeruhi wawili.
Kwa mujibu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, ndege aina ya Cessina 192
5H-FZS ikiwa na abiria watatu (3) na rubani 1 ilipata ajali wakati ikiruka
katika kiwanja hicho.
Katika ajali
hiyo askari wawili wamejeruhiwa na hali zao sio nzuri ambapo baada ya kuokolewa
walikimbizwa zahanati kwa ajili ya kupata huduma ya kwanza huku wakisubiri
ndege ya kuwapeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu
zaidi.
Aidha, miili
ya marehemu imehifadhiwa kwa muda katika zahanati ya hifadhi hiyo.
Rais Samia anawapa pole
wafiwa wote na anaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha
majonzi.
Mungu azilaze roho za
marehemu wote mahali pema peponi. Amina.
0 comments:
Post a Comment