Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza Mtoto Hamimu
Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye ni mkazi wa Nyakanazi
Mkoani Kagera. Mtoto huyo Hamimu alifika Ikulu kwa ajili ya kumshukuru Mhe.
Rais kwa msaada wa matibabu aliompatia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Jijini Dar es Salaam. Rais alimuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza wakati wa
Ziara yake Nyakanazi Mkoani Kagera tarehe 16 Oktoba, 2022 na kuagiza apatiwe
matibabu baada ya kuhangaika kwa muda mrefu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitazama maendeleo ya mkono wa Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye ni mkazi wa Nyakanazi Mkoani Kagera mara baada ya kuzungumza naye na kumpa Mkono wa Eid Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Samia aligharamia matibabu ya mtoto huyo kwa muda wa miezi sita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam
Hayawi Hayawi, huwa. Ndoto ya Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) aliokuwa akiililia kwa muda mrefu hatimaye imetimia. Mwanzo hakutanabahi kuwa aliye mbele yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, lakini baada ya kugundua alishikwa na hisia kali. Mtoto Hamimu alishikwa na butwaa pale ambapo Rais Samia alipojitambulisha kwake huku akiinama chini bila kuamini.
Mtoto huyo Hamimu alifika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumshukuru Mhe. Rais kwa msaada wa matibabu aliompatia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini humo.
Rais Samia alimuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza wakati wa Ziara yake ya Kikazi Nyakanazi Mkoani Kagera tarehe 16 Oktoba, 2022 na kuagiza apatiwe matibabu haraka baada ya kuhangaika kwa muda mrefu bila msaada wowote.
Mhe. Rais aligharamia matibabu yam toto huyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa muda wa miezi sita.
0 comments:
Post a Comment