Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, leo Aprili 03, 2023 amejumuika na Waumini mbali mbali wa Kiislamu, katika Ibada ya Sala ya Taraawehe, iliyofanyika Masjid Rahman, Msikiti uliopo Chamboni Micheweni.
Kabla ya Ibada hiyo, Alhaj Othman aliungana na viongozi mbali mbali wa Chama cha ACT Wazalendo wa kisiwani Pemba, katika Iftrari ya pamoja iliyofanyika katika makaazi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar yaliyopo Micheweni pia katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.











0 comments:
Post a Comment