Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu, Mhe George Simbachawene akizungumza na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI
walipokutana na TACAIDS wakati wa wasilisho la muundo na majukumu ya TACAIDS kwa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI katika Ukumbi wa Ofisi
za Bunge jijini Dodoma, Leo Machi,12, 2023.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Afya na Masuala ya UKIMWI, Stanslaus Nyongo akizungumza na wajumbe pamoja na watendaji wa TACAIDS
na Ofisi ya Waziri Mkuu waliohdhuria kikao cha kamati hiyo walipokutana leo
jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene na Katibu Mkuu Dkt. Jimmy Yonaz (kulia) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt Leonard Maboko alipokuwa
anawasilisha Muundo na Majukumu kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala
ya UKIMWI.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya
na Masuala ya UKIMWI, Mhe. Seif Salum Seif akichangia wakati wa kikao cha
kamati hiyo na TACAIDS kuhusu kubadilisha jumbe zinazotumika kwenye vibao vya ujenzi
vinavyo tumia maneno ya Unyanyapaa.
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI Mhe Hassan Mtega akichangia wakati wa kikao cha kamati hiyo umuhimu wa TACAIDS kufatilia utekelezaji wa majukumu ya kamati za UKIMWI za ngazi za chini.
**********
Na Nadhifa Omar, Dodoma.
Wairi wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe.George Simbachawene amesema Serikali kupitia
Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kutoa ushirikiano unaostahiki kwa kamati ya
Afya na masuala ya UKIMWI kutekeleza majukumu kwa kufuata miongozo,maoni na
ushauri unaotolewa na kamati hiyo.
Kauli hiyo amaitoa leo Machi12
,2023 baada ya Tume ya kudhibiti UKMWI Tanzania (TACAIDS) kuwasilisha Taarifa
kuhusu muundo na majukumu yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala
ya UKIMWI katika Ukumbi wa Ofisi za Bunge jijini Dodoma.
Awali akiwasilisha taarifa
hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko amesema TACAIDS ni
Idara inayojitegemea chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na imeanzishwa kwa mujibu wa
sheria Na.22 ya mwaka 2001 na Marekebisho yake Na.6 ya mwaka 2015, sheria hiyo
ni kwa ajili ya Tanzania Bara pekee. Zanzibar ipo Tume ya UKIMWI Zanzibar
(ZAC).
Dkt. Maboko ameyataja majukumu
ya TACAIDS kuwa ni kuandaa sera na miongozo kwa ajili ya mwitikio wa UKIMWI
nchini pamoja na kusimamia athari zake, kusimamia mpango mkakati kwa ajili ya
mipango ya programu za UKIMWI pamoja na masuala mtambuka yahusuyo virusi vya
UKIMWI na UKIMWI.
Kujenga mahusiano ya kitaifa
na kimataifa kwa watu wote wenye UKIMWI kwa kufanya uratibu wa masuala ya
UKIMWI,kutafuta raslimali fedha ,kuzigawa na kuzifuatilia katika programu za
Mwitikio wa UKIMWI,kusambaza taarifa kuhusu UKIMWI na madhara yake na programu
za kuzuia na kudhibiti.
Kukuza tafiti ,upashanaji
taarifa na kutunza kumbukumbu zinazohusiana na udhibiti wa UKIMWI nchini,kukuza
uraghibishi na utoaji wa elimu kwa ngazi ya juu kuhusu kuzuia na kudhibiti
UKIMWI, kufuatilia na kutathimini shughuli zote za UKIMWI zinazotekelezwa
nchini.
Aidha ameongeza kuwa shughuli
nyingine ni Kuratibu shughuli zote za UKIMWI na kuzisimamia kwa mujibu wa mkakati
wa Taifa wa UKIMWI, kwa kushirikiana na sekta binafsi husika kuwezesha juhudi
za upatikanaji wa tiba na kuhamasisha upatikanaji wa tiba na matunzo na chanjo.
Jukumu lingine ni kuhamasisha
haki na wajibu kwa watu wanaoishi na VVU ,kuhamasisha WAVIU kuishi kwa
matumaini na kushauri serikali kuhusu masuala yote yanayohusu kuzuia na
kudhibiti UKIMWI ,kutambua vikwazo katika utekelezaji wa kuzuia na kudhibiti
katika sera na programu ,kusimamia shughuli zote zinazohusiana na kuzuia na
kudhibiti maambukizi ya VVU na UKIMWI,pamoja na kushirikiana na sekta nyingine
husika,kufanya shughuli nyingine za kuzuia na kudhibiti VVU na UKIMWI.
Dkt. Maboko amesema
utekelezaji wa majukumu ya TACAIDS unaongozwa na sera ,sheria ,kanuni ,mikakati
na miongozo ikiwa ni pamoja na sheria ya tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania
Na,22 ya mwaka 2001na marekebisho yake Na6 ya mwaka 2015,Sera ya Taifa ya
UKIMWI ya mwaka 2001.
Mwongozo wa uraghibishi na
mabadiliko ya tabia,Mwongozo wa VVu na UKIMWI
na magonjwa sugu yasiyoambukiza, mwongozo wa kusshughulikia makundi
maalum kuhusu UKIMWI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ,mwongozo wa jinsia na
UKIMWI
,Mwongozo wa UKIMWI na haki za
binadamu ,Mwongozo wa kufundishia kamati za kudhibiti UKIMWI ngazi za
Halmashauri,kata na vijiji, pamoja na mwongozo wa kuunda kamati za kudhibiti
UKIMWI kwenye mikoa,mwongozo wa kuunda kamati za kudhibti UKIMWI kwenye
Halmashauri.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe
Stanslaus Nyongo iliipongeza TACAIDS kwa kazi kubwa waliyoifanya katika
kudhibiti na kupunguza maambukizi ya VVU nchini na kuagiza kuendelea kufanyia
kazi ushauri na maekezo yaliyotolewa na kamati hiyo,ikiwa ni pamoja na kufanya
ufatiliaji wa utekelezaji wa majukumu ya kamati za kudhibiti UKIMWI ngazi za
chini.
0 comments:
Post a Comment