Na Mwandishi Wetu,
Morogoro
Kamati ya kudumu ya
Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeipongeza Serikali kwa uwekezaji
unaotia matumaini katika Machinjio ya kisasa ya Nguru Hills na kuishauri
kuhakikisha nyama inayozaliswa katika kiwanda hicho inakubalika kimataifa ili
kupata soko la uhakika haswa kwa soko la nje ya nchi.
Hayo yalisemwa na
wajumbe mbalimbali wa kamati hiyo ya Bunge walipotembelea machinjio hayo ya
kisasa yaliyopo Mvomero mkoani Morogoro.
Mradi wa Machinjio ya Nguru
Hills unaendeshwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF)
kwa kushirikiana na Wabia wenza ambao ni Kampuni ya Eclipse Investiment LLC na Kampuni
ya Busara Investment LLP
“Hongereni sana tumeona kazi hii nzuri,
uwekezaji ni mzuri sana. Tunawapongeza, na pongezi za pekee kwa Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan, Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi zake
kubwa, tunamuombea nia yake nje kwa taifa letu ifanikiwe.Kwani uwekezaji huu ni
matokeo ya sera nzuri za serilkali yetu.” Alisema Bibi. Fatma Tawfiq,
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii.
Mwenyekiti huyo aliwataka wajumbe wa kamati
hiyo kwa pamoja kuhakikisha wanaishauri serikali na wawekezaji wengine ili
kiwanda hicho kithibitishwe kimataifa ili bidhaa zake ziweze kuuzwa katika soko
lolote ulimwenguni.
Kwa upande wake, Mjumbe
wa kamati hiyo ya Bunge, Mhe. Kabula Shitobelo alisema, “hongereni sana kiwanda ni kizuri sana tumekitembelea na
tumeona jinsi kinavyofanya kazi”.
Mjumbe mwingine Mhe.
Sophia Mwakagenda pamoja na kuridhishwa na uwekezaji huo ambao tayari umetoa
ajira kwa vijana 300 alishauri kuwepo na usimamizi mzuri ili kiwanda kiwe na tija
kwa taifa.
“Mradi huu unakwenda kuwa mkombozi mkubwa kwa
wafugaji na wajasiriamali na wakiutumia vizuri utawasaidia kuongeza kipato”
alisema Mjumbe mwingine Mhe. Neema Mwandabila.
Akijibu baadhi ya hoja
za wajumbe wa kamati hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba,
alisema katika kuhakikisha nyama ya Nguru inawafikia watanzania wengi kiwanda
kina mpango wa kufungua maduka katika maeneo mbalimbali na kwa kuanzia duka
limeshafunguliwa Morogoro mjini.
CPA. Kashimba alisema bidhaa zinazozalishwa
katika machionjio ya kisasa ya Nguru zinaandaliwa kwa kufuata misingi ya imani
za dini zote, hivyo walaji wasiwe na shaka na nyama inayotoka kiwandani hapo.
“Tunaishukuru kamati
kwa kuamua kusaidia katika mchakato wa kupatikana kwa kibali cha bidhaa za
kiwanda hiki kutambulimka kimataifa, kwa kweli tukipata ISO itakuwa rahisi sana
kuuza bidhaa zetu popote pale Duniani.” Alisisitiza CPA Kashimba.
Akihitimisha ziara
hiyo, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu
(Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) aliishukuru kamati kwa kazi kubwa ya
kukagua miradi iliyo chini ya Wizara hiyo na kwamba wamefarijika sana kwa ziara
ya kamati hiyo.
“Tunahakikisha
tunaendelea kusimamia kiwanda hiki ili fedha za wanachama zilizowekezwa hapa
zifanye kazi iliyotarajiwa na hatimaye faida ipatikane ili wanachama waendelede
kulipwa mafaoa yao” alisema Mhe. Ndalichako.
Meneja Mkuu wa
Machinjio ya kisasa ya Nguru yaliyoko Wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro, Bw. Eric Cormack (kulia) akitoa maelezo kwa wajumbe
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii juu ya utendaji kazi
katika machinjio hayo, wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya uwekezaji ya PSSSF Machi 14, 2023
Meneja Mkuu wa Machinjio ya kisasa ya Nguru, Bw. Eric Cormack akitoa maelezo kwa wajumbe Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii juu ya utendaji kazi katika machinjio hayo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (kulia), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatma Tawfiq (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (kushoto) na wajumbe wa Kamati hiyo wakiwasili kwenye Machinjio ya Kisasa ya Nguru Hills wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro Machi 14, 2023.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii
Bibi. Fatma Tawfiq (katikati) akizungumza kwenye majadiliano baada ya kutembelea
machiojio ya kisasa ya Nguru
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakiwasili
katika kiwanda cha machinjio ya kisasa Nguru, kilichopo Mvomero, mkoani
Morogoro.Wajumbe hao wameongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Fatma Tawfiq
(wa pili kushoto). Wajumbe hao walipokelewa na Mhe. Prof. Joyce Ndalichako,
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, (wa
tatu kutoka kushoto), CPA. Hosea Kashimba, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF (wa kwanza
kushoto), Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya PSSSF Bw. Rashid Mtima na Meneja Mkuu wa
Machinjio ya Nguru Bw.Erick Cormack (aliyeshika bahasha).
0 comments:
Post a Comment