Hayo yamebainishwa na Waziri wa Habari,
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye baada ya kuzindua
mnara wa mawasiliano wa kampuni ya Tigo wenye teknolojia ya 2G na 3G uliojengwa
kwa ruzuku kutoka UCSAF katika kata ya Noondoto wilaya ya Longido mkoani Arusha
leo Machi 5, 2023.
Waziri Nnauye amesema Serikali ya Rais Samia inaendelea kuhakikisha kila
mtanzania anafikiwa na huduma ya mawasiliano hasa jamii za pembezoni na maeneo
yasiyo na mvuto wa biashara kwasababu mawasiliano yanachochea ukuaji wa uchumi,
usalama na maendeleo ya mtu binafsi na nchi kwa ujumla.
Aidha, ametoa rai kwa wananchi hasa vijana kutumia huduma za mawasiliano
kwa ajili ya maendeleo kwani zikitumika vibaya zinaweza kusababisha athari kwa
jamii ikiwa ni pamoja na uharibifu wa maadili ya kitanzania.
Katika hatua nyingine Waziri Nnauye ameipongeza Kampuni ya simu ya Tigo kwa
kuanza kukopesha simu janja kwa wananchi ikiwa ni hatua ya kuhakikisha wateja
wao wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijiti.
Inakumbukwa kuwa mwishoni mwa mwezi Januari, 2023 Waziri Nnauye alitoa rai
kwa makampuni ya simu kuangalia uwezekano wa kuanza kukopesha simu janja kwa
wananchi na kulipa kidogo kidogo wakati
akizindua mnara wa mawasiliano mkoani Katavi.
"Tunajivunia utulivu wa kampuni ya
Tigo na kuwafikia watanzania hadi vijijini na pia kwa kuanza kukopesha
simu janja kwa wananchi kwa malipo ya shilingi 1000 kwa siku kwa mwaka mzima
ili wananchi waanze kutumia huduma" ,amezungumza Waziri Nnauye
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Selestine Kakele amewataka
wananchi wa jamii ya wafugaji katika kata ya Noondoto kutumia huduma za
mawasiliano kutafuta fursa ya masoko ya mazao ya mifugo, kuongeza kasi ya
shughuli za uchumi na kujiletea maendeleo.
Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Bi. Justina Mashiba amesema Mfuko huo ni
mfano wa ushirikiano baina ya Serikali na sekta binafsi (makampuni ya simu)
ili kufikisha huduma za mawasiliano
vijijini, maeneo ya pembezoni na yale yasiyokuwa na Mvuto wa Biashara.
"Katika mradi huu wa mnara wa mawasiliano katika kijiji cha Noondoto
UCSAF imetoa ruzuku ya shilingi milioni 104.9 kwa kampuni ya Tigo kwa ajili ya
kukamilisha ujenzi wa mnara wa mawasiliano katika kijiji cha
Noondoto",amefafanua Mashiba.
Uzinduzi huo umeshuhudiwa na Mbunge wa Londido na Naibu Waziri wa Madini
Mhe. Dkt. Steven Kiruswa, viongozi wa Wilaya ya Longido pamoja na wafanyakazi
wa Wizara hiyo, UCSAF na Kampuni ya simu ya Tigo.
Waziri Nape alitumia nafasi hiyo kuipongeza Kampuni ya Tigo kwa kuwajali wateja wao kwa kuanza kuwa kopesha simu janja
0 comments:
Post a Comment