Kwa mara ya kwanza tangu Tanzania ipate uhuru wake,
Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) linatarajia kupeleka mabondia wawili wanawake
katika mashindano ya ubingwa wa dunia kwa wanawake.
Mashindano hayo yatahusisha nchi zote duniani
wanachama wa chama cha ngumi cha Dunia (IBA) yanatarajiwa kufanyika katika mji wa New Delhi- India.
Hayo yameamuliwa na kupitishwa katika kikao cha kwanza
cha viongozi wa shirikisho la ngumi Tanzania kilichofanyika usiku wa leo tarehe
05 March 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Africa Human Rights Network (AHRN)
Mbezi Beach Dar es salaam.
Timu hiyo kwa sasa ipo kambini kwa mazoezi makali ya
kujiandaa na mashindano hayo ambayo ipo chini ya walimu wanaotambuliwa na chama
cha ngumi cha Dunia (IBA) wakiwa na daraja la nyota mbili ambao na Samwel
Batmani ( Kocha Mkuu) na Mohamed Abubakar( Kocha Msaidizi.
Mabondia ni Rahma Joseph Maganga na Beatrice Ambros
Nyambega.
Timu hiyo kwa sasa ipo katika kambi ya Pamoja katika
hosteli za AFRICA HUMAN RIGHTS NETWORK Mbezi Beach kwa ufadhili wao AHRN ambao
ni wamiliki wa hiyo hosteli.
Aidha Pamoja na mambo mengi ya kiutendaji
yaliyoongelewa katika kikao cha leo shirikisho la ngumi Tanzania (BFT)
limepanga kuongea na waandishi wa Habari Jumanne ya Tarehe 07 March 2023 kuanzia
saa tatu asubuhi katika Gym ya OASIS
CLUB iliyopo Mbezi Beach Dar es salaam. Ambapo tutazungumzia kuhusiana na
safari ya timu yetu ya taifa ya wanawake kwenda katika mashindano hayo ya
ubingwa wa dunia Pamoja na mipango mingine ya shirikisho la ngumi Tanzania
(BFT)
Tunatoa wito kwa vyombo vyote vya Habari kujitokeza
siku hiyo ili kujua mipango ya uongozi mpya wa BFT kwa jinsi ulivyojipanga kuleta
mabadiliko ya maendeleo ya mchezo wa ngumi Tanzania.
0 comments:
Post a Comment