Wanawake wengi wamehamasika kupeleka watoto wao shule, Kliniki, Kupanga mipango ya familia pamoja na masuala mbalimbali ikiwemo kushiriki katika masuala ya uongozi na vikao vya maamuzi mbalimbali katika jamii zao.
TASAF pia imesaidiwa wanawake kuwapa watoto wao lishe bora na wengi wao kujiamini hivyo kushiriki mambo muhimu kwa kujiingaza katika vikundi mbalimbali vya kijamii na kuwawezesha kuchangia maendeleo katika familia zao.
Hayo yameelezwa na Lilian Mugwe Afisa maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofika wilayani humo ili kuona shughuli mbalimbali zinazofanya na TASAF ambapo ameongeza kwamba wanawake wengi wanapokuwa na uwezo wa kipato wanaheshimika katika jamii zao.
Mpango huo pia umesaidia kupunguza unyanyasaji wa Kijinsia kwani wanawake hao wamekuwa na uwezo wa kujitafutia mahitaji yao kwa kufanya Biashara ndogo ndogo na kuepuka kuwa tegemezi kwa kuendesha mambo yao na familia kwa ujumla wake.
Aidha Lilian ameongeza kwamba kutokana na mafunzo wanayopata kupitia TASAF imewasaidia kujiamiani na hata wengine kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbali mbali za uongozi.
Hata hivyo bado hawana nguvu kwa kiasi kikubwa kwa sababu katika jamii yetu wanaume wamekuwa hawaamini kwamba mwanamke anaweza kuongoza jambo ambalo kwa kiasi fulani limekuwa likiwakwamisha wanawake.
0 comments:
Post a Comment