Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi
Dkt Batilda Salha Burian akizungumza na Wajumbe zaidi ya 500 wa Mkutano Mkuu wa
5 wa mwaka wa Chama Kikuu cha Ushirika Milambo (Urambo na Kaliua) uliofanyika
juzi Wilayani Kaliua, Mkoani Tabora,
Na Lucas Raphael,Tabora
MAKAMPUNI ya wazawa na ya kigeni yanayojishughulisha na ununuzi wa zao la tumbaku Mkoani Tabora yametakiwa kulipa kiasi cha shilingi bil 1.6 za mavuno ya msimu uliopita vinginevyo yatafikishwa mahakamani na kutaifishwa mali zao ili kuweza kufidia kiasi gharama kwa (Amcos).
Onyo hilo limetolewa na Mkuu
wa Mkoa huo Balozi Dkt Batilda Burian alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa 5 wa mwaka wa Chama Kikuu cha Ushirika Milambo uliofanyika jana
Wilayani Kaliua.
Alisema kwamba kampuni hizo
zitafikishwa mahakamani na kuifishwa mali zao kwani wanaonekani wazi hawataki
kulipa madai ya wakulima jambo ambalo serikali ya mkoa hawalikubali bali mkono wa sheria ndio
utaamua.
‘Kampuni yoyote ambayo
haijamaliza kulipa madeni ya wakulima ya msimu uliopita ilipe haraka
iwezekanavyo, la sivyo tutawafikisha mahakamani, haiwezekani uchukue tumbaku ya
mkulima halafu usimlipe’, alisema
Alisema kwamba wakulima
wamekuwa wavumilivu hivyo serikali ya mkoa inalibeba jambo hilo ili wakulima
waweze kupata haki yao ya msingi .
Hata hivyo mkuu huyo wa
mkoa wa Tabora aliyataka makampuni ya
ununuzi wa zao la kutumbaku mkoani hapa kuhakikisha yalipa madeni yao yote ya
nyuma kabla ya kuanza msimu mpya wa masoko ya zao hilo mwaka huu.
Alisema licha ya baadhi ya
makampuni kumaliza madeni yao hadi sasa baadhi ya vyama vya msingi (Amcos)
havijalipwa zaidi ya sh bil 1.6 za mavuno ya msimu uliopita na sasa tumbaku
imeiva na msimu mpya wa masoko unakaribia kuanza.
Balozi Dkt Batilda alibainisha
kuwa kilimo cha tumbaku ni kazi ngumu inayohitaji kujituma na uangalizi wa
karibu sana na usipohudumia vizuri shamba lako huwezi kupata tumbaku nzuri
yenye ubora unaotakiwa katika soko la dunia na yenye gredi ya juu.
Alisisitiza kuwa serikali
kupitia Wizara ya Kilimo imeendelea kufanya juhudi kubwa za kuboresha shughuli
za wakulima ikiwemo kutoa ruzuku ya pembejeo, na kutafuta wanunuzi wakubwa ili
tumbaku yote inayozalishwa inunuliwe.
Balozi Batilda alifafanua kuwa
katika msimu uliopita pekee jumla ya kilo mil 30 za tumbaku zilizalishwa na
wakulima na kuuzwa zote na kwa mwaka huu makisio yao ni kuzalisha kilo mil 60
na zitauzwa zote tena kwa bei nzuri.
Alitoa wito kwa viongozi wa
Ushirika na Amcos kuendelea kuhamasisha suala zima la upandaji miti katika
maeneo yao na kuhakikisha miti inayopandwa inaendana na ardhi ya eneo husika
kwa kuwa baadhi ya miti huathiri mazingira.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa waTabora, Hassan
Wakasuvi aliwataka viongozi wa Ushirika kuwa watetezi wa kweli wa wakulima na
kutowaibia fedha zao.
Alishauri wakulima kutunza
vizuri tumbaku yao na kuifunga vizuri katika mabelo baada ya kuvunwa ili
ikienda sokoni isitolewe kasoro yoyote, ipendwe na makampuni yote na kuuzwa kwa
bei nzuri.
‘Viongozi wa vyama vya msingi
shirikianeni, pendaneni, watendeeni wema wanachama wenu, acheni kuwaibia
wanachama wenu, alichokopa mkulima ndicho alipe si vinginevyo’, alisema.
Alisisitiza kuwa Chama Cha
Ushirika Milambo kilipaswa kuwa juu zaidi kuliko hata vyama vingine vilivyoko
katika Mkoa huo vya WETCU na IGEMBENSABO kwa kuwa kinazalisha kilo nyingi za
zao hilo na mazao mengine.
Mbunge wa Jimbo la Kaliua Aloyse Kwezi alisema
kwa mwaka jana pekee Wilaya yake ya Kaliua ilizalisha zaidi ya kilo mil 20 za
tumbaku kuliko wilaya nyingine lakini akasikitishwa na tabia ya baadhi ya
wanunuzi kutolipa kwa wakati.
Na Lucas Raphael,Tabora
MAKAMPUNI ya wazawa na ya kigeni yanayojishughulisha na ununuzi wa zao la tumbaku Mkoani Tabora yametakiwa kulipa kiasi cha shilingi bil 1.6 za mavuno ya msimu uliopita vinginevyo yatafikishwa mahakamani na kutaifishwa mali zao ili kuweza kufidia kiasi gharama kwa (Amcos).
0 comments:
Post a Comment