Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea juu ya umuhimu wa maeneo yote ya serikali kuwa na hati miliki ili kuondoa migogoro baina ya wananchi na serikali
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua maeneo ya kituo cha afya cha Mbondo na kuwaagiza ofisi ya ardhi kupima maeneo hayo
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua maeneo ya kituo cha afya cha Mbondo na kuwaagiza ofisi ya ardhi kupima maeneo hayo
**************
Na Fredy Mgunda, Nachingwea.
MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ameagiza idara ya ardhi kuhakikisha wanapima na kutoa hati miliki kwenye viwanja vyote vya serikali ili kuondoa migogoro ya ardhi kwa wananchi na serikali.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa kituo cha Afya cha Mbondo,Moyo alisema kuwa kumekuwa na migogoro mingi baina ya wananchi na serikali kutokana na tatizo la mipaka.
Moyo alisema kuwa zikitolewa hati miliki kwenye maeneo yote ya serikali kutatua na kuondoa kabisa migogoro ya ardhi na kuwaacha wananchi wakiendelea kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kiuchumi.
Aliagiza kwa maafisa ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kupeleka ofisini kwake taarifa ya utekelezaji wa agizo la kupima ardhi na maeneo yote ya serikali.
Moyo alisema kuwa anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutatua changamoto za wananchi kwa kutatua migogoro mingi ya ardhi.
Kwa upande wake afisa ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Kantu Juma alisema kuwa wameyapokea maagizo ya mkuu wa wilaya hiyo ya kwenda kupima maeneo ya serikali na kutoa hati miliki ili kuondoa migogoro baina ya wananchi na serikali.
0 comments:
Post a Comment