Mkuu wa Mkoa huo Balozi Dkt Batilda Burian wa Tabora akiwa na mkuu wa wilaya ya Sikonge Simoni chacha aliyevaa suti bluu bahari wakiwa na maafisa mbalimbali wilaya na mkoa huo.
Moja ya shamba liloathiriwa na Mvua kubwa ya upepo iliyoambatana na mawe na mkulima huyo kupata hasara kubwa
Mkuu wa Mkoa huo Balozi Dkt Batilda Burian wa Tabora akizungumza na wakulima wa zao la Tambaku wilayani Sikonge mkoani hapa .
Mkuu wa wilaya Simon Chacha akizungumza neno juu ya zao la Tumbaku mbele ya wakulima zao hilo wilayani humo.
Mwenyekiti wa chama cha kikuu cha ushirika wa zao la Tumbaku (WETCU) Hamza Kitunga akisistiza jambo mbele wa wakulima wa zao hilo.
Meneja mkuu wa Wetcu ltd,Samwel Jokea akitoa maelezo mbalimbali juu ya wakulima wa zao la Tumbaku .
Wakulima wa chama cha msingi Makonge wilayani Sikonge wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Burian.
***********
Mvua kubwa ya upepo iliyoambatana na mawe imeharibu zaidi ya
ekari 15 kati ya 75 za zao la Tumbaku zilizolimwa na kusababisha hasara kubwa
kwa baadhi ya wakulima wa Chama cha Msingi cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku
Ngulu, kilichopo kata ya Chabutwa, kijiji cha kipanga Wilaya ya Sikonge Mkoani
Tabora.
Wakizungumzia tukio hilo kwa masikitiko makubwa mbele ya
Mkuu wa Mkoa huo Balozi Dkt Batilda Burian baadhi ya wakulima ambao mashamba
yao yameharibiwa vibaya na mvua hiyo walieleza kuwa wamepata hasara kubwa.
Mshara Kitoli, mkulima mkazi
wa kijiji hicho alisema alikuwa amelima ekari 7 za zao hilo na alitarajia
kuvuna zaidi ya kilo 500 lakini mvua hiyo imemharibia mipango yake baada ya
ekari 4 kuharibiwa vibaya.
Mhanga mwingine Samson
Brighton, mkulima mkazi wa kijiji hicho alisema kati ya ekari 5 alizolima msimu
huu ekari 4.5 zimeharibiwa vibaya na majani yote ya mmea huo yametobolewa na
kuangushwa chini.
Alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa
wana majonzi makubwa, kwa kuwa walitarajia kupata kilo nyingi msimu huu
kutokana na maandalizi mazuri ya mashamba yao, kulima kwa wakati na kupata mvua
za kutosha, lakini sasa furaha yao imegeuka kuwa huzuni.
Mwenyekiti wa Chama Msingi
Ngulu (Ngulu Amcos) kilichoko katika kijiji hicho Gile Cheja, alisema mvua hizo
zimeathiri AMCOS hiyo kwa kiasi kikubwa sana kwani walilima jumla ya ekari 75
za zao hilo lakini ekari 15 zimeharibiwa vibaya.
‘Tumepata hasara kubwa kwa
uharibifu huu, sijui itakuwaje, tunaomba serikali iangalie namna ya kutusaidia,
tuna mikataba na tulishapewa makisio ya kilo zinazotakiwa kuzalishwa’, alisema.
Baada ya kutembelea kijiji
hicho na kujionea uharibifu uliotokea, Mkuu wa Mkoa, Balozi Batida aliaahidi
kuwasiliana na Mamlaka husika ya maafa ili kuangalia namna ya kuwasaidia.
Aidha alielekeza Bodi ya
Tumbaku, Chama Kikuu cha Ushirika wa wakulima wa tumbaku Mkoani hapa (WETCU
LTD) na Afisa Ushirika kukaa na wahanga ili kuangalia namna ya kuokoa tumbaku
iliyobaki.
Katika ziara hiyo Balozi
Batilda pia alitembelea wakulima wa kijiji cha Iyombakuzova katika kata ya
Misheni na kujionea jinsi tumbaku ilivyostawi vizuri baada ya kutumia mbolea ya
ruzuku iliyotolewa na serikali msimu huu.
Alipongeza juhudi kubwa
zilizofanywa na serikali ya awamu ya 6 kwa kuanzisha utaratibu wa kutoa ruzuku
ya mbolea kwa wakulima kwa kuwa itawasaidia kuboresha shughuli zao, kuongeza
uzalishaji na kuongeza mapato yao.
Aliwahakikishia kuwa serikali
ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inajali sana wananchi hivyo itaendelea kuweka
utaratibu mzuri wa upatikanaji pembejeo hizo ili kumaliza changamoto zilizopo.
0 comments:
Post a Comment