MBUNGE wa Jimbo la Chalinze ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwan Kikwete amegawa
piki piki sita kwa watendaji wa Halmashauri ya Chalinze, Mkoani Pwani.
Aidha mbali na kugawa piki piki hizo
zitakazosaidia utendaki kazi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo pia amepokea
vifaa tiba kwaajili vituo vya afya na zahanati za vijiji 11 ndani ya
Hamashauri.
Kikwete pia alitembelea kiwanda cha
kuzalisha marumaru kilichopo Chalinze mkoani pwani na kukagua maendeleo yake.
Akizungumza wakati wa kukabidhi piki piki
hizo, Kikwete amewataka watendaji hao kutumia vyombo hivyo kwa kuzingatia
makusudio ya kutolewa kwao.
“Watendaji katumieni vyombo hivi kama
vilivyo kusudiwa na si vinginevyo, mkawasikilize wananchi katika maeneo yenu na
kutafuta ufumbuzi wa changamoto zao,”alisema Kikwete.
Aidha amewataka wataalam wa afya katika
vituo vya afya na zahanati kutunza vifaa vyote walivyo kabidhiwa ili vikatumike
kwa walengwa kwa ufanisi.
Alisema kwa sasa kazi kubwa inaelekezwa
kituo cha Afya Miono ambapo kazi ya ujenzi wa miundo mbinu inapaswa kuwa
kipaumbele.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete akikata utepe tayari kukabidhi pikipiki kwa Watendaji wa Kata sita za Halamashauri ya Chalinze.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan
Kikwete akigawa vifaa tiba kwa vituo vya afya vya Kata ya kibindu na Msata
pamoja na zahani za vijiji 11.
akijulia hali wagonjwa baada ya kugawa vifaa tiba
Viongozi wa Kiwanda cha kuzalisha marumaru na kupatiwa maelezo ya maendeleo ya mradi
0 comments:
Post a Comment