Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya nafasi za uongozi katika Serikali kama ifuatavyo:
Rais Samia amemteua Balozi Hussein Othman Katanga (pichani) kuwa Balozi wa Tanzania mjini New York, nchini Marekani na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa.
Balozi Katanga anachukua nafasi ya Balozi Profesa Kennedy Gaston ambae uteuzi wake umetenguliwa.
Kabla ya uteuzi huu balozi Katanga alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Rais Samia amemteua Dkt. Moses Mpogole Kusiluka kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Kabla ya Uteuzi huo Bw. Kusiluka alikuwa Katibu Mkuu Ikulu.
Rais Samia amemteua Kamishna Diwani Athumani Msuya (pichani) kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya uteuzi huo Kamishna Diwani alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Rais Samia amemteua Bw. Said Hussein Masoro kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Kabla ya uteuzi huo Bw. Masoro alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Shughuli za Ndani wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Uteuzi huu unaanza mara moja.
0 comments:
Post a Comment