Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip
Mpango akihutubia Viongozi, Wananchi wa Pemba pamoja na Wanafunzi mara baada ya
Ufunguzi rasmi wa Skuli ya Msingi ya Kwale iliopo Wilaya ya Chakechake Mkoa wa
Kusini Pemba leo tarehe 09 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za
Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip
Mpango akihutubia Viongozi, Wananchi wa Pemba pamoja na Wanafunzi mara baada ya
Ufunguzi rasmi wa Skuli ya Msingi ya Kwale iliopo Wilaya ya Chakechake Mkoa wa
Kusini Pemba leo tarehe 09 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za
Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikata utepe
kuashiria Ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Kwale iliopo Wilaya ya Chakechake Mkoa
wa Kusini Pemba leo tarehe 09 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra
za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiweka jiwe
la msingi la ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Kwale iliopo Wilaya ya Chakechake
Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 09 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa
shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi ya mfano wa mlango unaopatikana Zanzibar kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Lela Muhammed Mussa mara baada ya Ufunguzi rasmi wa Skuli ya Msingi ya Kwale iliopo Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 09 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea
zawadi ya mavazi yanayovaliwa Kisiwani Pemba
kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Lela Muhammed Mussa mara baada ya Ufunguzi rasmi wa Skuli ya Msingi ya
Kwale iliopo Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 09 Januari
2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar.
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Kwale mara baada
ya ufunguzi wa shule hiyo leo tarehe 09 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa
shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika
picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya Ufunguzi rasmi wa
Skuli ya Msingi ya Kwale iliopo Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba leo
tarehe 09 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Miaka 59 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Wananchi na viongozi mbalimbali wakifuatilia Ufunguzi rasmi wa Skuli ya Msingi ya Kwale iliopo Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 09 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
************
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 9
Januari 2023 amefungua rasmi Skuli ya Msingi ya Kwale iliopo Wilaya ya
Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba. Ufunguzi wa Skuli hiyo ni miongoni mwa
shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanyika kuelekea Sherehe za Miaka 59 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Akihutubia mara baada ya ufunguzi wa Skuli hiyo,
Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Nane ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuifanya sekta ya elimu kuwa sekta ya kipaumbele kwa
kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo za upungufu wa Madarasa na Walimu pamoja
na kuzifanyia ukarabati skuli zote za zamani zilizopo Unguja na Pemba.
Aidha ameongeza kwamba Serikali
imedhamiria kuajiri walimu wapya hasa wa masomo ya Sayansi na Hisabati ili
kuhakikisha kuwa inapunguza
na
kuondoa kabisa uhaba wa walimu Zanzibar. Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imedhamiria kujenga
miundombinu mingine muhimu kama vile maabara ya sayansi na kompyuta, maktaba
pamoja na kuongeza idadi ya mabweni ili kuwawezesha watoto kupata muda mzuri wa
kusoma.
Aidha Makamu wa Rais amesema tangu
kipindi baada ya Mapinduzi matukufu,
Serikali imeendelea kuongeza skuli katika Mikoa yote pamoja na kuboresha
miundombinu ili kuhakikisha watoto wanapata elimu iliyo bora kwenye mazingira
mazuri na salama. Ameongeza
kwamba ni vyema kuhakikisha vijana wanarithishwa historia nzuri ya mapinduzi matukufu ili wafahamu
umuhimu wa kuyaenzi na kuyalinda.
Amesema viongozi wakiongozwa na Hayati Mzee Abeid Amani
Karume waliamua kufanya Mapinduzi ili kujikomboa na madhila ya kikoloni ambayo yalijaa
unyanyasaji na ubaguzi mkubwa ikiwemo
kupata elimu kiasi ambacho hata uhuru wa kujiletea maendeleo haukuwepo.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amewasihi wazazi,
walezi pamoja na wananchi wote kuhakikisha watoto wa kiume na wa kike wanaojiunga
na skuli za
msingi na sekondari wanamaliza masomo. Amesema si vema
kuwaruhusu watoto kukatisha masomo yao kwa sababu zisizo zozote zile. Ametoa wito kwa hatua
kali za kisheria kuchukuliwa kwa watakaobainika kufanya unyanyasi wa
kijinsia na kingono, kuoa au kusababisha mimba za utotoni. Pia amesisitiza jamii kushirikiana kwa pamoja
kulea watoto katika mila na desturi sahihi, maadili yaliyo mema na kushika mafundisho
ya dini ambayo yatawaepusha na maovu mengi katika jamii inayowazunguka.
Makamu wa Rais amesema mifarakano katika familia, vitendo
vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto pamoja na mmomonyoko wa maadili
katika jamii vinachangia kwa kiasi kikubwa watoto kutofikia malengo yao katika
maisha. Ametoa wito kwa kwa Watanzania wote kushirikiana kuhakikisha haki za
mtoto zinalindwa na kuchukua hatua pale ambapo watoto wananyimwa haki zao. Aidha
amesema ni muhimu Wizara husika kuhakikisha zinaimarisha Programu ya msaada wa ushauri
wa Kisaikolojia kwa watoto, familia na jamii katika ngazi zote ili kupunguza
athari na changamoto zinazotokea ndani ya familia na jamii zetu kwa ujumla.
Kwa
Upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Mheshimiwa Lela Muhammed Mussa amesema jumla ya skuli mpya 45
zimejengwa Unguja na Pemba ndani ya mwaka mmoja katika hatua za kuimarisha
sekta ya Elimu Zanzibar.
Waziri
Lela amesema lengo la Serikali ya
Mapinduzi ni kuona Zanzibar inazidi kuboreka kielimu na hivyo mikakati
madhubuti ya kuondoa wingi wa wanafunzi madarasani imewekwa ikiwemo kuandaa
utaratibu wa kuondokana na mfumo wa wanafunzi kusoma kwa awamu mbili.
Awali
akitoa taarifa ya ujenzi wa Skuli hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Khamis Abdulla Said amesema jumla
ya shilingi bilioni 2.5 zimetumika katika ujenzi wa skuli ikihusisha madarasa
21 na kuweza kuhudumia wanafunzi 1890 wanaosoma kwa wamu na hivyo kuondokana na changamoto ya mrundikano wa wanafunzi
ilikuepo hapo awali.
Pia
amesema Wizara ya Elimu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na ile ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania zinashirikiana kwa karibu kuhakikisha changamoto katika
sekta ya elimu zinaondolewa kwa lengo la kuboresha sekta hiyo.
Katika
Hafla ya Ufunguzi wa Skuli hiyo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imependekeza Skuli hiyo kupewa jina la Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango.
0 comments:
Post a Comment