Nafasi Ya Matangazo

November 01, 2022

Mkuu wa Chuo Cha Ulinzi cha Taifa Meja Jenerali Ibrahim Mhona akiwa kwenye mazoezi katika uwanja wa Golf wa Jeshi la Ulinzi La wananchi wa Tanzania Lugalo kujiandaa  na mashindano hayo.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Jacob Mkunda ( katikati) akiwa awenye picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi wa Malawi  Jenerali Vincent Nundwe (wakwanza kushoto) na Mkuu wa Majeshi Mstaafu  Jenerali George Waitara (wakwanza kulia) mara baada ya shindano la Mkuu wa Majeshi Oktoba Mwaka huu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Jacob Mkunda ( katikati) akiwa Kwenye picha ya Pamoja Na Mkuu Wa Majeshi Wa Malawi  Jenerali Vincent Nundwe (watatu kushoto) na Majenerali Wa Tnznaia na Malawi mara baada ya Shindano la Mkuu wa Majeshi Oktoba mwaka huu.
*************
Na Meja Selemani Semunyu.

Wachezaji 12 wa Klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara wanatarajiwa kuondoka leo (Jumatano kuelekea Lilongwe Nchini Malawi kushiriki mashindano ya Siku Nne ya  Mchezo huo.

Akizungumza wakati wa maandalizi ya Safari hiyo Mkurugenzi wa Michezo na Utamaduni wa JWTZ Kanali Martin Msumali alisema maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni Safari Alfajiri ya Jumatano.

“ Lengo la mashindano haya ni kudumisha  ushirikiano na Malawi na pia kuchangia fedha kwa ajili ya Maveterani wa Vita  wa malawi walipigana vita kuu ya pili ya Dunia” Alisema Kanali Msumali.

Kwa Upande wake Balozi na Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Ulinzi Job Masima ambaye ni miongoni mwa wanaokwenda katika Mashindano hayo alisma amejisikia furaha kupata nafasi hiyo muhimu kwa mashirikiano.

“ Ni nafasi Nzuri kushiriki Mashindano haya nishukuru jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kukubali Mwaliko huu anaamini Safari hii inamanufaa makubwa kwa Pande zote mbili.” Alisema Balozi Masima.

Kwa Upande wake Mchezaji Mwingine Brgedia Jenerali Mstafu Joseph Mbilinyi alisema ni mara ya pili ankwenda kushiriki lakini anaamini mashindano ya mwaka huu yatakuwa na msisimko wa namna yake.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo aliwataja wachezaji wataoshiriki kuwa ni Jenerali George Witara, Luteni Jenerali Ibrahim Mhona,Brigedia Jenerali Mstaafu Joseph Mbilinyi, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwogo.

 Aidha Kanali Martin Msumali, Meja Japhet Masai, Meja Selemani Semunyu, Kapteni Samwel Mosha  na Kapteni   Chediel Msechu.

 Mashindano haya yanafuatia mwaliko kutoka Jeshi la Malawi mara baada ya Viongozi wa Juu wa jeshi la Malawi kushiriki katika mashindano ya kombe la Mkuu wa majeshi Tanzania Oktoba Mwaka huu wakiongozwa na Mkuu wa majeshi wa Malawi Jenerali Vincent Nundwe.
Posted by MROKI On Tuesday, November 01, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo