Nafasi Ya Matangazo

November 17, 2022

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja Mradi wa BRT, Eng. Barakaeli Mmari (kulia), na Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Dar es salaam Eng. Harun Senkuku alipokagua Daraja la Chang’ombe na barabara ya BRT II toka Katikati ya Jiji – Mbagala KM 20.3 Jijini Dar es Salaam leo.

Mbunge wa Temeke Mhe. Doroth Kilave akielezea kuridhishwa kwake kutokana na kasi ya ujenzi wa Barabara ya BRT -II toka Katikati ya Jiji – Mbagala KM 20.3, wakati Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa alipokagua maendeleo ya ujenzi huo.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Meneja Mradi wa BRT, Eng. Barakaeli Mmari alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Barabara ya Kilwa katika Makutano ya barabara hiyo na ya Nelson Mandela Kurasini Jijini Dar es Salaam ambayo ujenzi wake unaendelea.
WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ameelezea kuridhishwa kwake na Ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo haraka – (BRT) sehemu ya Katikati ya Jiji kwenda Mbagala na kumtaka mkandarasi anaejenga Barabara hiyo kuhakikisha inakamilika kama ilivyo pangwa.
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Prof. Mbarawa amesema katika kipindi cha miezi mitatu kutoka sasa anatarajia barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 20.3 itakuwa imefunguliwa yote kwa matumizi.
 
“Nia ya Serikali ni kupunguza msongamano Dar es Salaam hivyo nakuagiza TANROADS na Mkandarasi kuhakikisha sehemu inayokamilika magari yaruhusiwe kuitumia wakati ujenzi unaendelea ili kupunguza msongamano na kuleta ufanisi katika huduma za usafiri na uchukuzi katikati ya jiji la Dar es Salaam,” amesisitiza Prof. Mbarawa.
 
Aidha amewataka madereva wa magari katika barabara ambazo ujenzi wake bado unaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wakandarasi ili kulinda usalama wa abiria, wajenzi na magari kwa ujumla.
 
“…Hatuitaji ajali zitokee hivyo tutii maelekezo ya wataalam wetu yenye nia ya kupunguza msongamano na kulinda usalama wa watu na magari,” amesema Prof. Mbarawa.
 
Prof. Mbarawa amesema ujenzi wa Barabara na Magaraja jijini Dar es Salaam unafanywa kwa awamu hivyo wananchi waendelee kuiunga mkono Serikali ili kufikia malengo tarajiwa yaliokusudiwa.
  
Kwa upande wake, Meneja Mradi wa BRT, Eng. Barakaeli Mmari amesema ujenzi wa Daraja la Juu sehemu ya Chang’ombe makutano ya barabara za Nyerere na Kawawa uko sahihi kulingana na usanifu wake, lengo ni kutoa nafasi katikati kwa magari yaendayo haraka.
 
Amezungumzia umuhimu wa raia wema kupata taarifa sahihi kwa  TANROADS pale wanapoona katika miradi hiyo kuna jambo linaloitaji ufafanuzi.
Naye Mbunge wa Temeke, Mhe. Doroth Kilave ameishukuru Serikali na kuipongeza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kutokana na kasi ya ujenzi wa miadi hiyo katika jimbo lake.
 
Takribani Shilingi Bilioni 262 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa Barabara ya kupunguza msongamano ya Kilwa na Daraji la Chang’ombe katika makutano ya Barabara za Nyerere na Kawawa jijini Dar es Salaam.
Posted by MROKI On Thursday, November 17, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo