Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja(Mb) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kibengu Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa kuhusu kushirikiana kudhibiti moto katika mashamba ya miti,wakati wa ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta katika Shamba la Miti Sao hill.
Mhifadhi Mkuu wa Shamba la miti la Sao Hill,Lucas Sabida akieleza jambo kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja(Mb) alipotembelea ofisi za Sao Hill Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja(Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta katika Shamba la Miti Sao hill kwenye Kijiji cha Kibengu Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
Kamati ya Mawaziri wa Kisekta ikiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Angeline Mabula (Mb) katika kikao na Mkuu wa Mkoa wa Iringa ilipofanya ziara mkoani humo.Kamati ya Mawaziri wa Kisekta ikiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Angeline Mabula (Mb) (katikati) katika picha ya pamoja ilipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa ajili ya ziara ya kutatua migogoro ya ardhi mkoani humo.
***************
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii,Mhe.Mary Masanja(Mb) amewataka wananchi Mkoani Iringa kushirikiana
katika kudhibiti matukio ya moto yanayojitokeza kwenye mashamba ya miti binafsi
na ya Serikali.
Ameyasema hayo leo katika
Kijiji cha Kibengu Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa wakati wa ziara ya Kamati ya
Mawaziri wa Kisekta katika Shamba la Miti Saohill.
"Niwaombe sana kila mtu awe mlinzi wa mwenzake, kama unaandaa shamba hakikisha unaangalia upepo unaelekea wapi ndipo uchome" amesisitiza.









0 comments:
Post a Comment