Nafasi Ya Matangazo

October 19, 2022

Na Mary Gwera, Mahakama
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 19 Oktoba, 2022 amemkabidhi nyenzo za kazi Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga, Mhe. Asha Mwetindwa aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni.

Akizungumza mara baada ya hafla fupi ya kumkabidhi nyenzo hizo ofisini kwake Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam, Jaji Mkuu, Mhe. Prof. Juma amempongeza Hakimu huyo na kumtaka kuzisoma kwa makini nyaraka alizomkabidhi ili aweze kufahamu na kujikumbusha mambo ya msingi ya kuzingatia katika utekelezaji wa kazi yake.

“Kwanza nikupongeze kwa kuaminika na hatimaye kuweza kuteuliwa kushika nafasi hii, mfumo umekutambua kwa kazi nzuri unayofanya na hivyo naamini utaweza, pia nasisitiza usome kwa makini nyaraka zote nilizokukabidhi kwakuwa zina mambo mengi yatakayokuongoza katika majukumu yako,” amesema Jaji Mkuu.

Kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo, Mhe. Asha alikuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Muleba ambapo alihudumu katika nafasi hiyo kwa miaka nane kuanzia tarehe 08 Juni, 2014 mpaka mwaka huu.

Kwa mujibu wa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma, Mhe. Asha aliajiriwa mwaka 2007 na ana uzoefu wa miaka 15 kazini, ambapo amefanya kazi katika vituo mbalimbali na hivyo ana Imani kuwa ana uwezo wa kutekeleza majukumu yake mapya ipasavyo.

Kwa upande wake, Mhe. Asha ameahidi kutekeleza majukumu yake mapya kwa weledi kwa kufuata sheria na miongozo iliyopo.

Hafla hiyo fupi imehudhuriwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma, Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Sylvester Kainda, Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Masjala Kuu, Mhe. Said Ding’ohi, Naibu Katibu wa Jaji Mkuu, Mhe. Venance Mlingi na Mhe. Jovine Bishanga, Katibu wa Msajili Mkuu.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kushoto) akimkabidhi nyenzo za kazi Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga, Mhe. Asha Mwetindwa (kulia) aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni. Hafla fupi ya kukabidhiwa nyenzo hizo imefanyika leo tarehe 19 Oktoba, 2022  ofisini kwa Jaji Mkuu Mahakama ya Rufani (T) jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mhe. Venance Mlindi, Naibu Katibu wa Jaji Mkuu.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma (aliyesimama) akiongoza hafla fupi ya kukabidhiwa nyenzo Hakimu Mkazi Mfawidhi mpya wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga, Mhe. Asha Mwetindwa. Aliyeketi mbele ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma na Viongozi wengine wa Mahakama walioshiriki katika hafla hiyo fupi.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Hakimu Mkazi Mfawidhi mpya wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga, Mhe. Asha Mwetindwa (kulia) aliyekabidhiwa nyenzo za kazi leo tarehe 19 Oktoba, 2022.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Hakimu Mkazi Mfawidhi mpya wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga, Mhe. Asha Mwetindwa (kushoto) aliyekabidhiwa nyenzo za kazi leo tarehe 19 Oktoba, 2022. Kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Hakimu Mkazi mpya wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga, Mhe. Asha Mwetindwa (wa tatu kushoto) mara baada ya kumkabidhi nyenzo za kazi leo tarehe 19 Oktoba, 2022. Wa tatu kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani, wa pili kulia ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma, wa pili kushoto ni Msajili ya Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Sylvester Kainda, wa kwanza kulia ni Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt na wa kwanza kushoto ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania-Masjala Kuu, Mhe. Said Ding'ohi.
Posted by MROKI On Wednesday, October 19, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo