Nafasi Ya Matangazo

October 31, 2022

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), pamoja na viongozi wengine wa Serikali akifungua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, jijini Dodoma.
Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakifurahi jambo mara baada ya hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege  cha Kimataifa  cha Msalato, jijini Dodoma. 

Wageni mbalimbali
Machifu wa Mkoa Dodoma, Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, pamoja na wananchi wakisilikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, jijini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Godfrey Kasekenya (katikati) pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakisilikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, jijini Dodoma. 
Muonekano mnara wa kuongozea Ndege wa uwanja huo utakavyokua baada ya kukamilika
Manaibu Waziri  Ridhiwani Kikwete (Kulia) na Anthony Mavunde pamoja na viongozi wengine wakifurahi jambo mara baada ya hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege  cha Kimataifa  cha Msalato, jijini Dodoma. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiondoka Msalato, jijini Dodoma katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa.

Posted by MROKI On Monday, October 31, 2022 No comments
 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ikiwa ni uwezeshaji kwa biashara bora changa za TEHEMA (digital startups)  kupitia programu ya uwezeshaji kwa vijana na wanawake ya benki hiyo inayofahamika kama "IMBEJU" ambayo imezinduliwa katika Kongamano la Sita la TEHAMA lililofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Ijumaa iliyopita. Wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib, Iddrisa Kitwana (watatu kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (wapili kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari, Mohammed Abdull (wakwanza kushoto),Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya TEHAMA, Prof. Leornad Mselle (wapili kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga. Picha zote na Othman Michuzi.

************
Ikiendeleza jitihada zake za kukuza ujumuishi wa kiuchumi nchini, Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Tume ya TEHAMA imezindua programu mpya ya uwezeshaji kwa vijana na wanawake wajasiriamali, Sh. bilioni 5 zatengwa.
 
Programu hiyo iliyopewa jina la ‘IMBEJU’ imezinduliwa katika kilele cha Kongamano la Sita la TEHAMA lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Golden Tulip na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na taasisi kutoka ndani na nje ya nchi.
Akielezea kuhusu programu hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema kupitia ‘IMBEJU’, benki hiyo itakuwa ikitoa mitaji wezeshi kwa vijana na wawawake wajasiriamali wenye biashara na mawazo bunifu.
 
Nsekela alisema kupitia programu hiyo vijana watakuwa wakiwasilisha mpango wa biashara zao, na mawazo bunifu kwa upande wa wanafunzi, kisha wataalamu wabobezi watakuwa wakichambua na kuidhinisha mtaji na mafunzo kulingana na vigezo.
 
“Katika programu ya IMBEJU tutakuwa pia tukitoa mafunzo ya usimamizi wa biashara, matumizi ya mifumo ya TEHAMA, elimu ya fedha na masoko, na usaidizi wa kuboresha bidhaa na mawazo bunifu,” alisema Nsekela.
Aliongezea kuwa Benki hiyo pia imeanzisha kituo maalum cha mafunzo na ubunifu wa biashara katika Makao Makuu ya zamani ya Benki hiyo mtaa wa Azikiwe jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kitasimamiwa kwa ushirikiano na Tume ya TEHAMA nchini.
 
“Katika programu za vijana wajasiriamali tumeweka mkazo mkubwa zaidi katika biashara zinazoanza katika sekta ya TEHAMA tukilenga zaidi kuchochea uchumi wa kidijitali. Biashara katika sekta nyengine pia zitakuwa zikipata uwezeshaji,” alifafanua. 
Kwa upande wa uwezeshaji wa wanawake wajasiriamali, Nsekela alisema Benki hiyo itakuwa ikifanya kazi na taasisi na mashirika yaliyojikita katika kufanya uwezeshaji kwa wanawake. Uwezeshaji utafanyika kwa vikundi na wajasiriamali mmoja mmoja.
 
Kwa kuanzia katika uzinduzi huo wa programu ya IMBEJU Benki ya CRDB imekabidhi jumla ya shilingi milioni 50 kwa Tume ya TEHAMA ikiwa ni uwezeshaji kwa biashara change katika sekta ya TEHAMA (digital startups).
Akizindua programu hiyo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuanzisha programu hiyo ya ‘IMBEJU’ akisema itasaidia kukuza ujumuishi wa kiuchumi kwa vijana na wanawake.
 
“Idadi kubwa ya watu hapa nchini ni vijana na wanawake. Licha ya hivyo ndio watu tegemezi zaidi kiuchumi. Serikali imekuwa ikiweka jitihada kubwa katika kuliwezesha kundi hili. Niipongeze Benki ya CRDB kwa kuunga mkono,” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga alisema wamejipanga vilivyo kuhakikisha programu ya ‘IMBEJU’ inakwenda kuchochea kwa kasi ukuaji wa biashara changa nchini.
 
IMBEJU inaenda sambamba na kauli mbiu ya “Leave No One Behind” ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SGD) 2030 inayosisitiza uwezeshaji kwa makundi yaliyotengwa na kukabiliana na ukosefu wa usawa katika fursa za kiuchumi.
 
 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza wakati akifunga Kongamano la Sita la TEHAMA lililofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Ijumaa iliyopita.
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Iddrisa Kitwana akizungumza wakati katika Kongamano la Sita la TEHAMA lililofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Ijumaa iliyopita.

Posted by MROKI On Monday, October 31, 2022 No comments

October 30, 2022

Na K-VIS Blog/Khalfan Said, Kisarawe
BODI ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (Gaming Board of Tanzania-GBT) imeteketeza mashine haramu za kuendeshea michezo ya kubahatisha (Slot Machines) zipatazo 300.

Sambamba na hilo watu Wanane (8) wako mikononi mwa vyombo vya kisheria wakihusishwa na mashine hizo.

Zoezi hilo lililoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa GBT Bw. James Mbalwe limefanyika Oktoba 28, 2022 kwenye eneo la kuteketeza vifaa vya kielektroniki lililoko Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.

“Katika jitihada za kudhibiti waendeshaji haramu wa michezo ya kubahatisha GBT iliendesha operesheni maalum kwenye mikoa ya Pwani, Lindi, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Morogoro, Manyara na Songwe na kufanikiwa kukamata mashine hizo zenye thamani ya shilingi Milioni 300.” Alifafanua Bw. Mbalwe.

Alisema mashine hizo zilikamatwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufanya biashara bila ya Leseni ya GBT, mashine kuingizwa nchini bila ya kufuata taratibu za kisheria, kufanya biashara kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi au hayajakaguliwa na kuthibitishwa na Bodi (GBT) pamoja na  kukwepa kulipa kodi na tozo mbalimbali.

“Mashine hizi pekee zimepelekea serikali kukosa mapato yake kiasi cha shilingi Milioni 33 kwa mwezi sawa na shilingi Milioni 400 kwa mwaka, jambo hili halikubaliki.” Alisisitiza.

Pia Bw. Mbalwe alisema waendeshaji hao haramu ndio ambao wamekuwa wakiruhusu watu wenye umri usioruhusiwa kucheza michezo hiyo,

“Operesheni hii ni endelevu na itakuwa ikifanyika mara kwa mara ili kudhibiti vitendo hivyo na kuhakikisha michezo ya kubahatisha inaendeshwa kwa kuzingatia misingi ya kisheria na kuleta tija katika maendeleo ya Taifa letu bila ya kusababisha athari hasi au madhara yoyote kwa jamii yetu.” Alisisitiza.

Aidha Mkurugenzi Mkuu huyo aligusia pia hatua ya hivi karibuni ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Yasinta Mboneko ya kuzuia biashara ya michezo ya kubahatisha katika wilaya yake baada ya kubaini kwamba kulikuwa na uvunjfu wa sheria ambapo alielekeza jeshi la jadi Sungusungu kusimamia agizo hilo.

“Sisi kama chombo cha serikali chenye dhamana ya kusimamia michezo ya kubahatisha, tunaona hatua aliyochukua ni nzuri na itasaidia katika kuimarisha utekelezaji wa sheria, lakini nashauri wakati mwingine ili zoezi hilo lifanyike vizuri ni vema viongozi na mamlaka nyingine wakashirikisha GBT ambayo ina watu wenye weledi katika eneo hilo na kwahakika itarahisisha utekelezaji wake bila ya kuleta taharuki.” Alisema. 

Alisema “GBT tumeamua kupambana na uhalifu wa mashine za michezo ya kubahatisha zilizozagaa kwenye maeneo yasiyoruhusiwa na kutozingatia sheria, hata kama watakuwa ni waendeshaji tuliowapa leseni tutachukua hatua kali pindi tutakapobaini wamevunja sheria.” Alionya Bw. Mbalwe.

Pia alisema GBT inaendelea na msako wa kuwabaini wale wote wanaoingiza mashine hizo nchini kinyume cha sheria.

Nae Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni ya Chilambo ambayo ndiyo inahusika na kuharibu “taka hatarishi” hususan za umeme, Bi. Venither Gideon alisema mashine hizo zitavunjwa vunjwa na kisha kuzitenga kwenye makundi kulingana na asili yake.

“Jukumu letu ni kuhakikisha tunaziharibu mashine hizi katika njia ambayo ni salama kwa uhifadhi wa mazingira.” Alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa GBT Bw. James Mbalwe (kulia) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) sehemu ya shehena ya mashine haramu za kuendeshea michezo ya kubahatisha (Slot Machines) zipatazo 300, zikiteketezwa huko Kisarawe Mkoani Pwani Oktoba 28, 2022
Bw. Mbalwe na maafisa wa GBT wakizikagua mashine hizo muda mfupi kabla ya zoezi la kuziteketeza kuanza.
Mkurugenzi Mkuu wa GBT Bw. James Mbalwe, akizunguzma na waandishi wa habari kwenye eneo la tukio.
Mkurugenzi Mkuu wa GBT Bw. James Mbalwe (wapili kulia), Meneja wa Ukaguzi na Udhibi GBT, Bw. Sadiki Elimsu (watatu kulia) na Afisa Habari na Elimu kwa Umma, Bi. Zena Athumani (kulia), wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni ya Chilambo, Bi. Venither Gideon, muda mfupi kabla ya kuanza kwa uteketezaji wa mashine hizo.
Meneja wa Ukaguzi na Udhibi GBT, Bw. Sadiki Elimsu (kushoto) akizungumza jambo mbele ya Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni ya Chilambo, Bi. Venither Gideon (katikati) na Afisa Habari na Elimu kwa Umma GBT,  Bi. Zena Athumani
Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni ya Chilambo, Bi. Venither Gideon, akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la tukio.
Zoezi la kuziteketeza mashine hizo likiendelea.
Posted by MROKI On Sunday, October 30, 2022 No comments



 

Posted by MROKI On Sunday, October 30, 2022 No comments

October 28, 2022

Shirika linalojihusisha na utoaji elimu ya fedha nchini, DSIK Tanzania limekabidhi mahitaji mbalimbali ikiwemo mabegi, madaftari (Counter Books), kalamu na tauro za kike katika Shule ya Sekondari Nyakurunduma jijini Mwanza.

Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi mahitaji hayo lililofanyika Oktoba 27, 2022, Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo Stephen Safe alisema hatua hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Akiba Duniani ambayo huadhimishwa wiki ya mwisho ya mwezi Oktoba kila mwaka.

Alisema mahitaji hayo yatawasaidia wanafunzi 80 ambao ni wanachama wa Klabu ya Akiba iliyoanzishwa na shirika la DSIK Tanzania katika Shule ya Sekondari Nyakurunduma ili kujifunza kwa ufasaha elimu ya fedha hukU tauro/pads zikiwasaidia wanafunzi wa kike kutokosa masomo wakati wa hedhi.

Safe aliwahimiza wanafunzi kuwa na mtazamo chanya kuhusu masuala ya fedha, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, kujiwekea malengo na kutunza akiba ili kutimiza malengo hayo akisema "weka akiba leo ili kesho yako iwe imara"

Naye Mkufunzi wa Elimu ya Fedha Shirika la DSIK Tanzania, Rukia Amin alisema shirika hilo linatoa elimu ya fedha kupitia Klabu za Akiba katika Shule za Msingi na Sekondari zipatazo 90 jijini Mwanza ili kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya fedha hususani kuweka akiba wangali bado wadogo ambapo kwa mwaka 2021/22 zaidi ya wanafunzi elfu saba wamenufaika na elimu hiyo.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyakurunduma akiwemo Petro Leston na Mariam Zacharia walisema Klabu ya Akiba imewajengea uelewa kuhusu masuala ya kifedha hususani utaratibu wa kutunza akiba kupitia fedha za matumizi wanazopewa na wazazi na pia kuanzisha shughuli za ujasiriamali ikiwemo ufugaji wa kuku na sungura wangali bado shuleni hatua itakayowajenga kwa maisha ya baadae.

"Klabu ya Akiba imetuwezesha kutunza akiba tofauti na hapo awali ambapo tulikuwa tukipewa hela ya matumizi ya shule tunatumia yote. Tunawashukuru sana DSIK Tanzania kwa kutupatia elimu ya fedha na pia mahitaji ya shule ikiwemo mabegi na madaftari, hatutawaangusha kwani tutasoma kwa bidhii ili tutimize malengo yetu" alisema Glory Ehad na Samwel Mihayo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mkazi wa shirika la DSIK Tanzania, Stephen Safe (kushoto) akikabidhi mahitaji ya shule ikiwemo mabegi, madaftari, kalamu pamoja na taulo za kike kwa wanafunzi wanaoshiriki Klabu ya Akiba katika Shule ya Sekondari Nyakurunduma jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkazi wa shirika la DSIK Tanzania, Stephen Safe akizungumza kwenye zoezi fupi la kukabidhi mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi wanaoshiriki Klabu ya Akiba katika Shule ya Sekondari Nyakurunduma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Akiba Duniani 2022.
Mkurugenzi Mkazi wa shirika la DSIK Tanzania, Stephen Safe akizungumza wakati wa zoezi hilo.
Mkufunzi wa Elimu ya Fedha kutoka Shirika la DSIK Tanzania, Rukia Amin akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi mahitaji ya shule kwa wanafunzi 80 wanaoshiriki Klabu ya Akiba katika Shule ya Sekondari Nyakurunduma jijini Mwanza.
Mwakilishi kutoka Shirika la DSIK Ujerumani, Fabian Partsch akitoa salamu zake.
Wanafunzi wanaoshiriki Klabu ya Akiba katika Shule ya Nyakurunduma wakifuatilia hafla hiyo.
Wanafunzi wa Nyakurunduma Sekondari jijini Mwanza.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Mwanachama Klabu ya Akiba Nyakurunduma Sekondari jijini Mwanza, Petro Leston akieleza umuhimu wa elimu ya akiba.
Mwanachama Klabu ya Akiba Nyakurunduma Sekondari jijini Mwanza, Mariam Zacharia akieleza mahitaji yaliyotolewa na shirika la DSIK Tanzania yatakavyowasaidia kujifunza.
Mwanachama Klabu ya Akiba Nyakurunduma Sekondari jijini Mwanza, Samwel Mihayo akizungumzia umuhimu wa elimu ya fedha kwa wanafunzi mashuleni.
Mwanachama Klabu ya Akiba Nyakurunduma Sekondari jijini Mwanza, Glory Ehad akitoa shukurani kwa shirika la DSIK Tanzania kwa kuwasaidia mahitaji ya shule.
Mwalimu Fatina Kayela wa Shule ya Sekondari Nyakurunduma jijini Mwanza ambaye pia ni Mwalimu wa Klabu ya Akiba shuleni hapo alisema Klabu hiyo imetoa ari kwa wanafunzi kujifunza elimu ya fedha.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyakurunduma jijini Mwanza wakiwa na vifaa mbalimbali vya shule ikiwemo mabegi waliyokabidhiwa na shirika la DSIK Tanzania.
Posted by MROKI On Friday, October 28, 2022 No comments
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Jukwaa la Kibiashara kati ya Tanzania na Korea kwenye hoteli ya Mondrian iliyopo Seoul nchini Korea, Oktoba 28, 2022.
Balozi wa Tanzania nchini Korea Togolani Mavura akizungumza wakati alipomkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua Jukwaa la Kibiashara kati ya Tanzania na Korea kwenye hoteli ya Mondrian iliyopo Seoul nchini Korea, Oktoba 28, 2022.
 Baadhi ya washiriki wa Jukwaa la Kibiashara kati ya Tanzania na Korea wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Jukwaa hilo kwenye hoteli ya Mondrian iliyopo Seoul nchini Korea, Oktoba 28, 2022
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya washiriki wa Jukwaa la Kibiashara kati ya Tanzania na Korea kwenye hoteli ya Mondrian iliyopo Seoul nchini Korea, Oktoba 28, 2022. 
Posted by MROKI On Friday, October 28, 2022 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo