Nafasi Ya Matangazo

September 05, 2022

Mahakama ya Juu nchini Kenya leo itatoa uamuzi wake juu ya shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais wa mnamo Agosti 9 ambao Naibu Rais wa nchi hiyo William Ruto alitangazwa mshindi kwa idadi ndogo ya kura. 

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ndiye aliyefungua shauri mahakamani akidai kuwepo hitilafu kwenye uchaguzi huo ambao kwa sehemu kubwa ulifanyika kwa utulivu kabla ya kutokea mparaganyiko wakati wa kutangazwa matokeo. 

Muda mfupi kabla ya Ruto kutangazwa mshindi, tume ya uchaguzi nchini humo iligawika na baadhi ya wajumbe wake walitangaza kujitenga na matokeo yaliyotolewa wakisema kulikuwa ukiukwaji wa taratibu na ukosefu wa uwazi. 

Baada ya wiki mbili za kusikiliza hoja za kila upande, mahakama ya juu nchini Kenya, ambayo miaka mitano iliyopita iliiufuta uchaguzi mwingine wa urais, leo mchana itatangaza uamuzi wake unaosubiriwa kwa shauku kubwa.
Posted by MROKI On Monday, September 05, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo