Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na
Michezo Bw. Saidi Yakubu akimkabidhi Mhe. Simon Sirro Balozi wa Tanzania nchini
Zimbabwe vitabu vya kufundishia Kiswahili Septemba 20, 2022 Mtumba, Mji wa
Serikali jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na
Michezo Bw. Saidi Yakubu akimkabidhi Mhe. Luteni Generali Mathew Mkingule
Balozi wa Tanzania nchini Zambia vitabu vya kufundishia Kiswahili Septemba 20,
2022 Mtumba, Mji wa Serikali jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na
Michezo Bw. Saidi Yakubu akimkabidhi Mhe. Caroline Chipeta Balozi wa Tanzania
nchini Uholanzi vitabu vya kufundishia Kiswahili Septemba 20, 2022 Mtumba, Mji
wa Serikali jijini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akiongea na Mabalozi Septemba
20, 2022 Mtumba, Mji wa Serikali jijini Dodoma; Mhe. Simon Sirro Balozi wa
Tanzania nchini Zimbabwe (watatu kushoto), Mhe. Caroline Chipeta Balozi wa
Tanzania nchini Uholanzi (wa kwanza kushoto) na Mhe. Luteni Generali Mathew
Mkingule Balozi wa Tanzania nchini Zambia (wa pili kushoto). Wa pili kulia ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu.
Na Eleuteri Mangi, WUSM
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) imewapatia vitabu Mabalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Zambia na Malawi ambavyo ni nyenzo ya kubidhaisha lugha ya Kiswahili katika nchi mbalimbali duniani.
Mabalozi hao ambao wamefanya ziara y Wizarani Dodoma leo Septemba 20, 2022 ni Mhe. Simon Sirro Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Caroline Chipeta Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi na Mhe. Luteni Generali Mathew Mkingule Balozi wa Tanzania nchini Zambia.
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) imewapatia vitabu Mabalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Zambia na Malawi ambavyo ni nyenzo ya kubidhaisha lugha ya Kiswahili katika nchi mbalimbali duniani.
Mabalozi hao ambao wamefanya ziara y Wizarani Dodoma leo Septemba 20, 2022 ni Mhe. Simon Sirro Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Caroline Chipeta Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi na Mhe. Luteni Generali Mathew Mkingule Balozi wa Tanzania nchini Zambia.
Vitendea kazi walivyokabidhiwa ni vitabu vya vya kufundishia lugha ya Kiswahili ikiwemo Kamusi Kuu ya Kiswahili Toleo la Tatu la 2022, Mwongozo wa Kufundisha Kiswahili kwa Wageni pamoja na kitabu cha Furahia Kiswahili ambavyo vyote ni nyenzo ya kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili katika nchi wanazoenda kufanyakazi.
Akizungumza na Mabalozi hao Ofisini kwake Mtumba Mji wa Serikali jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul amesema Mabalozi hao wameipa lugha ya Kiswahili kipaumbele, ndiyo maana wameona ni vema kabla ya kwenda kwenye vituo vyao vya kazi wafike Wizarani kupata nyenzo za kufanyika kazi ili kueneza lugha hiyo kwenye nchi walizopangwa kufanyakazi.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu amewahimiza Mabalozi hao kuwa wawakilishi wa nchi kwa kuhakikisha wanaongeza mikataba (MOU) ya kufundisha Kiswahili katika nchi wanazokwenda kufanya kazi vikiwemo vyuo vikuu vya nchi hizo, kuhimiza kuanzishwa kwa vituo vya kufundisha Kiswahili, kutumia programu tumizi ya TEHAMA kufundisha Kiswahili inayojulikana “Swahili Prime” pamoja na kuwahimiza Watanzania kutumia fursa ya lugha ya Kiswahili katika nchi hizo ikiwemo ukalimani.
Kwa upande wake Mhe. Caroline Chipeta Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi kwa niaba ya Mabalozi waliofika Wizarani hapo amesema kuwa Tanzania ndiyo msingi wa lugha ya Kiswahili, hivyo wanawajibu wa kukikuza na kukibidhaisha Kiswahili kwa kuwa ni kipaumbele cha Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, Balozi Mhe. Chipeta
ameongeza kuwa watatumia fursa hiyo kuanzisha madarasa ya kufundishia Kiswahili
kwenye vituo vyao vya kazi ili kuongeza kasi ya kukuza na kuieneza lugha ya
Kiswahili duniani.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Utamaduni Dkt. Emmanuel Temu, Mkurugenzi Msaidizi Dkt. Resani Mnata pamoja na
Katibu Mtendaji wa BAKITA Bi Consolata Mushi wamehudhuria kikao hicho.
0 comments:
Post a Comment