Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (pichani juu) ametoa wito kwa wanaparokia wa Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni jijini Dar es Salaam, kushiriki katika Sensa ya Watu na Makazi itakayo fanyika tarehe 23 mwezi Agosti
2022.
Akiongea wakati wa Harambee ya
kutegemeza Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni ambayo imeabatana na kilele
cha Sikukuu ya Mavuno leo tarehe 24, Jijini Dar es Salaam, amesisitiza kuwa
zoezi la sensa ni muhimu kwa Taifa katika kupanga mipango ya maendeleo.
“Serikali yetu ikiwa na idadi kamili ya watu wa makundi mbalimbali ili
kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinagawiwa kulingana na mahitaji, hivyo
niwasihi watu wote tujiandae kuhesabiwa”
Aidha, katika hatua nyingine Mhe. Ndalichako amewapongeza wanaparokia hao
hususani wanajumuiya ambao wamevuka malengo ya kukusanya michango kwa ajili ya
kutegemeza Parokia yao, hivyo amewasihi waendelee kujiwekea hazina kwa
Mwenyezimungu.
“Kila mmoja wetu atoe kwa ajili ya Mwenyezimungu, ukitoa kwa ajili yake unakuwa
umeiweka hazina yako katika mahala salama, tunapo toa tusiangalie thamani ya
kitu bali thamani ya uwekezaji kwa Mwenyezimungu”
Kwa upande wake Baba Paroko wa Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni, Padri
Gallen Mvungi amewasihi wanaparokia hao kuendelea kushkamana na kushirikiana
katika kutoa michango ili waweze kufikia malengo ya makusanyo waliyoyaweka kwa
mwaka huu.
Shughuli ya Kutegemeza Parokia hiyo imefanyika siku ya kilele cha Sikuu ya
Mavuno ikiwa na ujumbe kutoka Zab:50-54, Mtolee Mungu Dhabihu za kushukuru,
Mtimizie aliye juu Nadhiri zako.
0 comments:
Post a Comment