Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Maaskofu kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika pamoja na baadhi ya viongozi katika maadhimisho ya mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) uliofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Julai, 2022.
Maaskofu wa Kanisa Katoliki kutoka nchi mbalimbali pamoja na Wageni wengine wakiwa kwenye maadhimisho ya mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) uliofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Julai, 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsalimia Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Muadhama Kardinali Polycarp Pengo kwenye maadhimisho ya mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) uliofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Julai, 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewataka Viongozi wa dini na kisiasa
pamoja na waumini kuhakikisha wanadumisha amani na kutunza mazingira nchini.
Rais Samia ametoa wito
huo leo wakati wa maadhimisho ya mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza
ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) akisisitiza kuwa uwepo wa amani nchini unasaidia kutunza
ikolojia.
Aidha, Rais Samia
amesema uharibifu wa mazingiza kama ukataji miti huathiri hali ya hewa duniani ikiwemo
kina cha bahari hivyo ni wajibu wetu kulinda mazingira ili kutohatarisha maendeleo
yetu.
Rais Samia pia amesema
hatuna budi kutunza vyanzo vya maji na misitu, kupanda miti na kuhakikisha mazingira
ya maeneo yanayotuzunguka yanasafishwa katika miji yote kama inavyoelekezwa kwenye
Sera ya Taifa ya Mazingira.
Kwa upande mwingine, Rais
Samia amesema Serikali ya Tanzania inafuata siasa ya maendeleo jumuishi (inclusive
development policy), hivyo ipo tayari kuzipokea na kufanya kazi na taasisi
zisizo za kiserikali zikiwemo za kidini na kijamii ili kufikia mustakabali
mwema wa maisha na maendeleo ya mwanadamu.
Rais Samia ametoa wito
kwa Viongozi wa kidini kuendelea kutekeleza kwa vitendo Malengo Endelevu 17 ya Dunia
na Malengo ya Umoja wa Afrika (AU) ikiwemo utunzaji wa mazingira.
0 comments:
Post a Comment