Nafasi Ya Matangazo

June 17, 2022

 Mfanyakazi wa Airtel Tanzania kutoka idara ya Utumishi, Rose Shitindi akichangia damu kwa furaha leo ambapo watumishi wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania Ofisi ya Makao Makuu, Morroco Dar es Salaam walijitolea kuchangia damu katika Mpango wa Taifa wa Damu Salama. Anaemhudumia ni Muuguzi, Peter Chami kutoka Huduma ya Taifa ya Damu Salama. Wafanyakazi wa Airtel  wameshiriki katika mpango wa uchangiaji damu ili kuokoa maisha ya watu wanaohitaji damu.Afisa Muuguzi, Peter Chami kutoka Huduma ya Taifa ya Damu Salama akimhudumia Meneja Mauzo wa Airtel Tanzania, Wainduni Mushi wakati wa uchangiaji damu leo Juni 17,2022 katika ukumbi wa Airtel Makao Makuu Morroco jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi wa Airtel  wameshiriki katika mpango wa uchangiaji damu ili kuokoa maisha ya watu wanaohitaji damu.

Meneja Biashara wa Airtel Tanzania David Nsimba akihudumiwa na Afisa Muuguzi, Peter Chami kutoka Huduma ya Taifa ya Damu Salama wakati wa uchangiaji damu leo ​Juni 17,2022 ​katika ukumbi wa Airtel Makao Makuu Morroco jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi wa Airtel  wameshiriki katika mpango wa uchangiaji damu ili kuokoa maisha ya watu wanaohitaji damu.


Afisa Muuguzi, Peter Chami kutoka Huduma ya Taifa ya Damu Salama akimsaidia mfanyakazi wa Airtel Tanzania kutoka kitengo cha Mtandao, Gabriel Mshiu wakati akichangia damu katika Makao Makuu ya Airtel Morocco jijini Dar es Salaam leo Juni 17,2022. Wafanyakazi wa Airtel  wameshiriki katika mpango wa uchangiaji damu ili kuokoa maisha ya watu wanaohitaji damu.
***********

KAMPUNI ya Simu ya Airtel Tanzania leo imeungana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya mapo wa kampuni hiyo kurudisha huduma kwa Jamii (CSR).

 Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uchangiaji huo wa damu, Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Airtel Tanzania, Stella Kibacha amesema uchangiaji damu ni moja ya

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa zoezi hilo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Airtel Tanzania Stella Kibacha, alisema kuwa kuchangia damu ni dhamira ya kampuni katika kuhudumia na kusaidia jamii.

“Tumesukumwa kushiriki katika mpango wa leo wa uchangiaji damu kwani ni wazi  kwamba kumekuwa na hitaji la damu katika benki ya damu salama ili kuhudumia maisha ya watu…Tunafuraha kuwa wafanyakazi wa Airtel wameamua kuchangia damu kwa hiari na pia kuhamasisha marafiki na familia kufanya hivyo jijini Dar es laam na maeneo mengine nchini ili kuokoa maisha ya watu wanaohitaji damu” alisema Kibacha.

Kibacha amesema kauli mbiu ya kimataifa ya mwaka huu ni “Kuchangia damu ni kitendo cha mshikamano”. Tanzania kupitia Mpango wa Taifa wa Damu salama (NBTS) inahitaji damu kila siku kwa ajili ya Huduma za matibabu na dharura za Afya.

Alisema Airtel Tanzania inajivunia kuandaa zoezi la uchangiaji damu kwa wafanyakazi wake na kuonyesha mshikamano katika kuadhimisha siku ya uchangiaji damu.

 “Tunawashukuru wote wanaochangia damu na wote ambao huchangia damu kila inapowezekana ili kuokoa maisha ya watu na kuhimiza sana watu wengi zaidi nchini kuchangia damu kwa hiari na mara kwa mara,” alisema Kibacha.

 Kwa mujibu wa takwimu za NBTS, Tanzania inahitaji uniti 550,000 za damu kwa mwaka kwa ajili ya Huduma za dharura za Afya lakini kwa mujibu wa NBTS mwaka jana waliweza kukusanya uniti 331,279 tu za damu, ambapo kwa takwimu ni asilimia 70 tu ya damu inayohitajika kwaajili ya kuokoa maisha ya watoto, mama wanaojifungua, wagonjwa wa saratani, na wale majeruhi katika ajali mbalimbali zinazohatarisha maisha.

Posted by MROKI On Friday, June 17, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo