Mmwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania
(UWT) Taifa Gaudentia kabaka akiwa na zawadi ya kikombe cha chai chenye picha yake ambayo hubarika kila wakati kikiwa na chai kinatokea picha yake kisipokuwa na chai kinakuwa cheusi
Mmwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania
(UWT) Taifa Gaudentia kabaka akipokea tuzo ya uongozi bora kutoa kwa viongozi wa UWT Iringa
***************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania
(UWT) Taifa Gaudentia kabaka
amewapomgeza UWT mkoa wa Iringa kwa ujenzi wa nyumba za makatibu na
kukiimarisha chama na kuongeza ushirikiano baina ya serikali na chama cha
mapinduzi (CCM)mkoa wa Iringa.
Akizungumza wakati wa ziara ya siku mbili mkoani
Iringa,Kabaka alisema kuwa uongozi wa umoja huo umefanikisha kukituliza chama
cha mapinduzi kutokana na utulivu uliopo kwenye jumuiya hiyo.
Kabaka alisema kuwa viongozi wa UWT mkoa wa Iringa
wamekuwa viongozi imara katika kuiongoza jumuiya hiyo ndio maana wamekuwa na
umoja na mshikamano katika uongozi.
Alisema kuwa kwa mara ya kwanza miaka mitano ya
uongozi wake amefanikisha kuongeza idadi ya wabunge wa viti maalum kuwa wengi
bungeni.
Kabaka alisema kuwa sasa ni wakati sahihi wa
kuchagua viongozi ambao wataweza kuiongoza jumuiya hiyo na kuendelea kuwa imara
kwa ustawi wa chama cha mapinduzi.
Alisema kuwa wanawake wote wenye sifa za kugombea
nafasi mbalimbali ndani ya jumuiya hiyo wachukue fomu na wagombee kwa ajili ya
kuingoza na kuikuza jumuiya hiyo.
Kabaka alisema kuwa chama cha mapinduzi
kinautaratibu mzuri wa kuwachuja viongozi wanaotaka kugombea hivyo amewataka
kuondoa wasisi wa kugombea nafasi mbalimbali ndani ya UWT
Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudentia kabaka
amewashukuru kabila la wahehe kwa kumvisha nguo za kihehe ambazo zimemuongezea
heshima kubwa katika uongozi wake.
Alisema kuwa amefurahi kuvishwa vazi hilo ambalo
kwa miaka mingi amekuwa anaona kwenye tv tu historia ya chief mkwawa hivyo
ameahidi hata livua vazi hilo hadi amalize ziara mkoa wa Iringa na ataendelea
kulivaa mara kwa mara.
Lakini pia mwenyekiti wa UWT Taifa aliwashukuru UWT
mkoa wa Iringa kwa tuzo na zawadi mbalimbali ambazo amepewa leo mkoa wa Iringa
kuwa hatawasahau wema wao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT mkoa wa
Iringa,Niocolina Lulandala alisema kuwa wanampongeza mwenyekiti wa UWT Taifa
Gaudentia kabaka kwa
kuijenga ofisi ya UWT ambayo idara zote za jumuiya hiyo zinapatikana makao
makuu ya chama jijini Dodoma hivyo kwa miaka yake mitano amefanya maendeleo
makubwa kwenye umoja huo.
Lulandala alisema kuwa mwenyekiti wa umoja huo
amefanikiwa kuunganisha jumuiya ya UWT kuwa na umoja na ushirikiano ambao
umesadia kuongeza wananchi chama wapya na kukisaidia chama kufanya vizuri
kwenye nyanja mbalimbali za utawala.
Alisema kuwa wameendelea na ujenzi wa nyumba za
watumishi wa jumuiya ya UWT mkoa wa Iringa ambazo zitawasaidia kuacha kupanga
mtaani zote hizo kuunga mkono juhudi za mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudentia
kabaka katika kuhakikisha watumishi wote wanaishi kwenye nyumba zao
Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudentia kabaka
amekabidhiwa tuzo ya umahiri katika kuiongoza jumuiya ya UWT taifa kwa
kuiwezesha jumuiya hiyo kuwa na umoja na ushirikiano katika kukikuza chama cha
mapinduzi.
Naye mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga alisema
kuwa chama cha mapinduzi CCM Iringa wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na
serikali ndio maana mkoa wa Iringa umetulia na unafanya kazi za kimaendeleo.
Alisema kuwa serikali ya mkoa wa Iringa umetoa
zaidi ya bilioni kwenye mfuko wa akina mama wa asilimia 4 na wamejipanga
kuhakikisha mwaka ujao wa fedha wataongeza zaidi ya hapo.
Sendiga alisema kuwa serikali ya awamu ya sita
imefanikiwa kuwatua ndoo wanawake wa mkoa wa Iringa kwa kuleta miradi mingi ya
maji kila wilaya na halmashauri zake.
Alisema kuwa Iringa bado kunachamoto ya ukatili wa
kijinsia hivyo serikali ya mkoa wa Iringa imeanza kuwafunga watu wote ambao
wamekuwa wanafanya vitendo vya kikatilii.
Sendiga alisema kuwa wananchi wa mkoa wa Iringa
waache mara moja tabia ya kuwaficha wananchi ambao wamekuwa walifanya vitendo
vya ukatili wa kijinsia ili serikali ichukue hatua stahiki kwa watuhumiwa hao.
Mwenyekiti wa cham cha mapinduzi (CCM) mkoa wa
Iringa Dkt Abel Nyamahanga alisema kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga
amekuwa kiongozi bora kuiongoza Iringa kuleta maendeleo ya wananchi.
Dkt Nyamahanga alisema kuwa chama cha mapinduzi CCM
mkoa wa Iringa kimemteua mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga kuwa balozi wa
kupinga vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia mkoa wa Iringa.
Aidha Dkt Nyamahanga alisema kuwa wanachama wote wa
CCM mkoa wa Iringa wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya
chama hicho bila uoga wowote ule.
Alisema kuwa CCM mkoa wa Iringa itawachukulia hatua
kali watu wote ambao wameanza kampeni mapema na wale ambao wamekuwa wakitoa na
kupokea rushwa ili wapate uongozi.
Nyamahanga alisema kuwa Iringa wataendelea kuunga
mkono juhudi za mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM taifa ambaye ni Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kila jambo ambalo
amekuwa akilifanya kuleta maendeleo kwa watanzania.
0 comments:
Post a Comment